LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKOA WA SIMIYU KUJIKITA NA UTENGENEZAJI WA BIDHAA ZA NGOZI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Mkoa wa Simiyu utajikita katika uwekezaji na  utengenezaji wa bidhaa  mbalimbali  hususani za  ngozi ikiwemo mipira kwa ajili ya kuuza na kuwasaidia wajasiriamali wadogo na kati kujiinua kiuchumi.

Hayo yalisemwa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka alipotembelea Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO)Mwanza na Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) tawi la Mwanza, kwa ajili ya kujionea shughuli zinazofanywa,ili  kujifunza na kuyafanyia kazi kwa vitendo katika mkoa wake, ikiwa ni juhudi za ushawishi wa Meneja wa SIDO Damian Chang'a wakati alipomtembelea mkoani kwake hivi karibuni.

Mtaka mara baada ya kutembelea na kujionea shughuli zinazifanywa  na kiwanda cha Mwanza Quality Wines kilichopo ndani ya SIDO, aliahidi kuanzisha kiwanda kama hicho mkoani Simiyu ambacho kitatumia malighafi tofauti, ili kuingia katika soko la ushindani.

Aidha aliahidi, kuanzisha kiwanda kwa ajili ya bidhaa za ngozi na watajikita zaidi katika utengenezaji wa mipira ili kuinua uchumi wa mkoa na wajasiriamali mkoani humo, hii ni baada ya kukagua na kujionea namna DIT wanavyotengeneza na kuzalisha bidhaa kwa kutumia ngozi za wanyama.

Kwa upande wake Chang' a alisema, SIDO ipo kwa ajili ya kuwezesha wajasiriamali wadogo na wa kati pamoja na viwanda vidogo na vya kati,pia wanamatawi   katika mikoa ya Tanzania Bara isipokuwa mkoa wa Simiyu na Songwe, hivyo alitumia fursa hiyo kumshawishi Mtaka kutembelea  shirika na taasisi hiyo ili kujionea shughuli zinazofanyika.

Vilevile alisema, shirika hilo  tangu kuanzishwa kwake, limeweza kutoa mafunzo ya stadi mbalimbali kwa wajasiriamali, ambao wengi wao wamefanikiwa   na kuweza kujiinua kiuchumi na kujiajiri na kuajiri wengine, ambapo alitolea mfano kiwanda cha Mwanza Quality Wine ambapo mmiliki wake  ametokea mikononi mwa SIDO huku akianza na mtaji wa 500,000 na mpaka sasa anamtaji wa sh bilioni moja.

Naye Mkurugenzi wa Mwanza Quality Wines Leopord Lema aliwaomba, wajasiriamali kutokukata tamaa bali waendane na hali ya biashara,mpaka sasa ni miaka 9 tangu kuanzia kiwanda hicho na alianza na mtaji wa laki tano ila sasa anamtaji wa bilioni moja pamoja na kuajiri wafanyakazi 24.

Aidha alisema, lengo lake baaada ya miaka 3, akipata eneo atajenga kiwanda kikubwa nchini kitakachozalisha wine.
Kadhalika Mkuu wa Chuo cha DIT Albert Mmari alisema, taaluma wanayotoa ni yakuwezesha viwanda vidogo kuanzia ngazi ya familia, vijiji,wilaya mpaka taifa,hivyo mkoa wa Simiyu pia unaweza kutengeneza mipira na watoto wakaacha kuchezea ya makaratasi.

No comments:

Powered by Blogger.