LIVE STREAM ADS

Header Ads

TIMU ZA SOKA ZA IBUNGILO NA BUGOGWA ZATINGA FAINALI YA LIGI YA ANGELINE ILEMELA JIMBO CUP.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Timu ya Kata ya Ibungilo na Bugogwa zilizopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza, zimefuzu kuingia fainali za   ligi ya Angeline Ilemela Jimbo Cup, inayotarajia kutimua vumbi Novemba sita mwaka  katika uwanja wa CCM Kirumba.

Timu ya Ibungilo iliibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya wapinzani wao timu ya Shibura,katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali   wa ligi hiyo uliochezwa juzi kwenye uwanja CCM Kirumba.

Hata hivyo timu ya Ibungilo  ilipata ushindi huo uliiopelekea kufuzu kuingia fainali kupitia mshambuliaji wake Credy Duru(8), aliyefunga goli dakika ya 43 kipindi cha kwanza huku Mtesigwa Benedictor (16) akiipatia goli la pili timu hiyo dakika ya 76 kipindi cha pili.

Naye Kocha wa timu ya Ibungilo Swala Daudi alisema timu yake ni nzuri na anashukuru imepata nafasi ya kufuzu fainali,pia timu hiyo ina majeruhi nmoja ambaye ni Credy Duru aliyepata majeraha katika mguu, ila anaimani mpaka siku ya fainali atakuwa amepona.

Pia katika mchezo wa pili wa nusu fainali uliochezwa jana katika uwanja wa CCM Kirumba, Bugogwa iliibuka na ushindi wa goli 5-2 dhidi ya timu ya Kitangiri.

Aidha katika mchezo wa fainali wa ligi hiyo, utawakutanisha timu ya Ibungiro na Bugogwa, huku timu zote zikitambiana kuibuka na ushindi.

Kwa upande wake Mratibu wa ligi hiyo  Almas Moshi,alisema ligi hiyo imedhaminiwa na Mbunge wa jimbo la Ilemela Angelina Mabula, ambapo mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha shilingi milioni moja,huku wapili akipata laki tano na mshindi wa tatu ataondoka na fedha tasmilu laki tatu.

No comments:

Powered by Blogger.