LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAARIFA KUHUSU UKAMATAJI WA BANDIA ULIOFANYWA NA MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA NCHINI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvatory, BMG Dar
Dawa bandia zisizofaa kwa matumizi ya binadamu zimekamatwa katika baadhi ya maeneo ya Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini baada ya ukaguzi maalum wa kusaka dawa bandia uliofanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA).

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Hiiti Sillo ametanabaisha hayo wakati akitoa taifa ya matokeo ya ukaguzi maalum wa dawa uliofanyika katika mikoa ya Kanda ya  Ziwa na Nyanda za Juu Kusini.

“Kutokana na ukaguzi maalum tulioufanya katika Kanda hizo kutafuta dawa bandia na zisizo sahihi kwa matumizi ya binadamu tumefanikiwa kukamata dawa bandia aina tano ambazo zipo kwenye makundi mawili ya Dawa za malaria na Viua vijasumu(Antibiotics)” alisema

Aidha Sillo alisema kuwa ukaguzi huo maalum umeweza kusaidia kukamata dawa ya malaria aina ya vidonge vya Quinine ambayo inadaiwa kutengenezwa katika kiwanda cha Elys Chemical nchini Kenya na nyingine zinatengenezwa hapa nchini katika kiwanda cha Shelys Phamaceuticals Ltd.

Alisema kuwa pamoja na kukamata dawa bandia pia zoezi hilo lilifanikiwa kubaini na kukamata dawa zilizoisha muda wa matumizi , zisizosajiliwa zenye ubora duni zenye thamani ya Tsh. Milioni 17.463.

Aliongeza kuwa Ukaguzi huo ulitokana na kuwa na taarifa za awali ambazo zilionyesha uwepo wa dawa bandia katika maeneo ya Geita na Mara mwezi Agosti na Septemba mwaka huu na kusistiza kwamba zoezi hilo la ukaguzi linaendelea nchini  kote na watakaokutwa  na hatia watachukuliwa hatua stahiki.

Kwa upande wake Msajili wa Baraza la Famasia Elizabeth Shekalaghe, alisema kuwa wataalamu wa madawa watakaokutwa na hatia ya kusambaza na kuhudumia dawa bandia watafutiwa usajili na kuacha kutoa huduma kwa mujibu wa sheria ya dawa , chakula na vipodozi.

“Wataalamu wa dawa ambao wanasambaza na kuhudumia dawa bandia watafutiwa usajili na kuacha kutoa huduma kwa mujibu wa sheria ya dawa , chakula na vipodozi pindi watapogundulika” alisema Bi. Shekalaghe.

Pamoja na hayo alisema kuwa ukaguzi huo ulianza Oktoba 4 mwaka huu na unafanywa kwa ushirikiano wa TFDA, Jeshi la polisi na Maafisa kutoka Baraza la Famasia Tanzania na litakuwa endelevu.

No comments:

Powered by Blogger.