LIVE STREAM ADS

Header Ads

MTIFUANO WA MASHINDANO YA ANGELINE ILEMELA JIMBO CUP 2016 WAANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Mashindano ya  ligi ya Angeline Ilemela Jimbo Cup yamezinduliwa rasmi juzi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilemela, John Wanga, huku timu ya Buswelu Fc ikikubali kichapo cha goli 1-0 dhidi ya watani wao wa jadi Nyakato Fc.

Mchezo huo ambao ulikua ni wa ufunguzi wa ligi hiyo, uliyochezwa katika uwanja wa shule ya msingi Buswelu, na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali,huku Buswelu wakiwa ni wenyeji na kushindwa kufurukuta kwa wapinzani wao Nyakato Fc ambayo walifunga goli dakika ya 5 kipindi cha kwanza kupitia mshambuliaji wake  Msabaha Mahela.

Wanga aliwaomba wachezaji wa timu zinazoshiriki mashindano hayo, kuzingatia taratibu na sheria za mpira ,ili kutekeleza dhamira ya serikali ya awamu ya tano ya michezo ni ajira.

Pia alisema, kupitia juhudi za Mbunge wa Jimbo hilo Angelina Mabula anaamini wilaya hiyo itafanya vizuri katika michezo kuanzia ngazi ya mkoa nakutoa timu nyingi zitakazo shiriki ligi kuu Tanzania.

Naye Katibu wa Mbunge wa Jimbo hilo Kheri James alisema, fursa walioipata ya kuanzishwa kwa ligi hiyo, iwe chachu ya  kuinua na  kuleta tija katika michezo ndani ya  wilaya  ya Ilemela.

Kwa upande wa Mratibu wa Mashindano ya ligi ya Angeline Ilemela Jimbo Cup Almas Moshi alisema, ligi hiyo itatimua vumbi ndani ya siku 20, katika viwanja mbalimbali ikiwemo Magomeni,Kona ya Bwiru,Buswelu, Kayenze, Sabasaba na Bugogwa.

Hata hivyo alisema,  timu 19, kutoka Kata zote zilizopo wilayani humo  ndio zinazoshiriki ligi hiyo ambazo ni Buswelu, Ilemela, Nyamanoro, Bugogwa,Nyamong'oro, Nyakato, Kahama,Mecco,Shibula,Kayenze,Sangabuye,Buzuruga,Nyasaka,Kiseke,Kawekamo,Pasiansi,Ibungiro,Kitangiri na Kirumba.

Aidha aliongeza kuwa, ligi hiyo imegawanyika katika makundi manne, huku kundi A,B,C  kila moja kuwa na timu tano na kundi D zikishiriki timu 4.

Vilevile Kocha wa timu ya Nyakato Fc Faisal Hau alisema vijana wanauwezo,hivyo wadau wengine wajitokeze kuunga mkono juhudi za Mbunge huyo pamoja na ligi hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.