LIVE STREAM ADS

Header Ads

SERIKALI KURASIMISHA MAKAZI NCHI NZIMA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Displaying picha ya waziri lukuvi 2.JPGNa James Salvatory BMG-Dar
Serikali imesema ina mkakati wa wa kurasimisha makazi nchini kwa kupanga na kumilikisha ardhi katika makazi yasiyopangwa ili kusadia kupunguza makazi holela.

Hayo yalisemwa jana Jijini Dar es salaam na Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Wiliam  Lukuvi, katika maadhimisho ya siku ya makazi dunia.

Lukuvi alisema kazi ya urasimishaji inaendelea katka jiji la Dar es salaam katika maeneo ya Kimara, Chasimba na Makongo Juu hadi mwezi uliopita, viwanja 4,818 vilikuwa vimetambuliwa ambapo viwanja 4,665 vimepimwa na maandalizi ya umilikishaji  yanaendelea.

Aidha amesema urasimishaji unatarajiwa kuanza kufanyika katika Manispaa za Musoma, Kigoma, Tabora, Sumbawanga, Singida na Lindi lengo ni kulasimisha makazi yasiyopungua 100,000 kwa mwaka huu.

“Natoa rai kwa mamlaka za upangaji miji kuhakikisha kwamba zinaweka miundombinu na huduma za jamii katika maeneo mapya ya makazi  nay ale yanayolasimishwa ili kwenda sambamba na kaulimbiu ya mwaka huu" Alisema Lukuvi.

Kwa upande wake mratibu wa  mradi  wa urasimishashi wa ardhi, Lyidia Bagenda, alisema mradi huo unashirikisha wananchi wa eneo husika.

Nao wanachi wa Kata ya Kilungule iliyopo kimara jijini Dar es salaam, wamepongeza hatua hiyo ya Serikali na wameomba urasimishaji huo uweze kuwafikia wananchi wote nchini.

No comments:

Powered by Blogger.