LIVE STREAM ADS

Header Ads

VITENDO VYA UKATILI KWA WATOTO VYAZIDI KUONGEZEKA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvatory BMG Dar
Imeelezwa kuwa vitendo vya ukatili kwa watoto pamoja na kukithili kwa vitendo vya biashara ya uchagudo vimeongezeka kwa kasi.

Hayo yelisemwa jana na Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Shirika la Railway Children, Peter Kent, wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo alisema katika utafiti waliofanya katika mkoa wa Mwanza umebaini kuwa watoto ambao hukumbwa na vitendo vya ukatili katika umri mdogo. 

Huku ikonyesha kuwa zaidi ya wasichana 418 katika mkoa huo wanajihusisha na biashara ya uchangudoa ambapo kati yao wasichana 218 wanaofanya biashara hiyo ni wanawake wenye umri chini ya miaka 18.

Pia imebainika kuwa zaidi ya 19,40 ya watoto ndani ya mkoa wa Mwanza  wanaishi katika mazingira magumu na hatarishi.

"Mara nyingi  hali hiyo husababisha mzunguko wa umasikini zaidi na kuwa katuka hatari zaidi na matokeo hasi ya kimaisha, ambapo utafiti unaonesha asilimia 100 ya watoto wa mitaani wamewahi kunyanyaswa kimwili au maneno, huku asilimia ya wasichana na asilimia 25 ya wavulana wamedhalilishwa kijinsia,"alisema

Kent alizitaja takwimu za utafiti huo kuwa watoto 1940 huishi na kufanya kazi mitaani katika Jiji la Mwanza likiwa ni ongezeko la asilimia 25 tangu mwaka jana, katika miezi 12 tu idadi ya wasichana wanaofanya biashara ya ngono kwa asilimia 229.

Huku akidai kuwa hilo ni  ongezeko kubwa likiwa ni la wasichana wenye umri kati ya miaka 11-14, Ambapo idadi ya wasichana wanaofanya biashara ya ngono ni 418 na kati ya hao 218 ni wenye umri wa chini ya miaka 18, pia amefafanua kuwa kumekuwepo kwa kupungua kwa asilimia 40 ya watoto wa mitaani kati ya miaka 0-14 kwa kipindi cha miaka mitatu kwa walengwa.

"Sababu za watoto kuishi katika Mazingira Magumu na kupelekea kufanya mambo yasiyostahili kuwa ni umasikini, unyanyasaji na kutelekezwa, ambapo licha ya juhudi za Serikali, wao tumeamua kuandaa kongamano la kimataifa walilolipa jina la 'Kuvunja Mzunguko' litakalofanyika November 17 na 18 mwaka huu katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania na kutoa fursa ya ushiriki wa wajumbe 250 ambao kwa pamoja watajadiliana namna ya kuvunja mzunguko na kupata uelewa mkubwa wa mikakati iliyothibitika ya kuvunja mzunguko wa ukatili kwa familia dhidi ya watoto wanaoishi mitaani," aliongeza

No comments:

Powered by Blogger.