WAZIRI WA AFYA AITAKA TFDA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUHUSU MFUMO WA KIELEKRONIKI WA UTOAJI TAARIFA ZA MADHARA YA DAWA.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Na James Salvatory, BMG Dar
Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia na watoto, Ummy Mwalimu, ameitaka Mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na mfumo mpya wa kielektroniki wa utoaji taarifa za madhara ya dawa.
Akizungumza jana Jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa mfumo wa kielekitroniki wa utoaji wa taarifa za madhara ya dawa, Waziri Mwalimu alisema mfumo huo utawezesha watendaji wa afya ,wagonjwa na wananchi kutoa taarifa za madhara yanayohisiwa kusababishwa na matumizi ya dawa hivyo ni vema wananchi kupewa elimu kuhusu mfumo huu na kujipanga kuweka mfumo huu kwenye simu za kawaida ili kila mwenye simu aweze kuitumia
Aidha waziri aliwasihi tfda kushirikia na sido ambao wana dhamana ya kuendeleza viwanda vidogo vidogo kwa ajiri ya kuwasaidia wajasiliamani wadagowadago ambao wanazozalisha bidhaa kuwa salama
Naye Mkurugenzi wa TFDA, Profesa Hiiti Sillo, alisema mfumo huo utakuwa ni wa kieletroniki ambao utakuwa kwenye simu na kompyuta zilizounganishwa kwenye mtandao (internet) kwa kupita tovuti ya TFDA ambayo ni www.tfda.go.tz/adr
Aidha alisema kabla ya kuzindua mfumo huu wameweza kufanya majaribio katika mwezi juni hadi agosti 2016 na kuweza kupokea taarifa za madhara ya dawa zipatazo 36 na hivyo kuongeza taarifa zinazopokelewa.

No comments: