LIVE STREAM ADS

Header Ads

FOUNDATION KARIBU TANZANIA WATAKA UKATILI WA MAJUMBANI UTOKOMEZWE NCHINI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Viongozi mbalimbali nchini wakiwemo wa  dini  na siasa wametakiwa  kukemea vitendo vya ukatili  majumbani wanaofanyiwa watoto, ili  kukomesha na kutokomeza vitendo hivyo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa  shirika lisilo la kiserikali  linalojishughulisha na  kupinga ukatili dhidi ya watoto majumbani  Foundation Karibu Tanzania (FKT) Benard Makachia, katika mafunzo ya kupinga ukatili kwa viongozi mbalimbali, yaliyofanyika kwenye uwanja wa shirika hilo,lililipo wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.

Makachia alisema, ili kukomesha ukatili dhidi ya watoto, viongozi mbalimbali wakiwemo wa dini na siasa kwa nafasi zao,wanatakiwa kukemea na kuelimisha jamii kupinga vitendo hivyo.

Pia  alisema, jamii inapaswa kutoa taarifa  kwa vyombo vya dora juu ya ukatili  majumbani   ili kuweza kuchukua sheria dhidi ya watu hao.

Aidha aliwaomba,  wazazi na walezi   kuwaelimisha watoto wao, kutambua  haki na wajibu wao kwa jamii na taifa Kwa ujumla.

“Nawaomba wazazi na viongozi wa dini  kutoa taarifa pindi mtakapo sikia kuna mzazi anafanya  vitendo vya ukatili kwa watoto,ili kumchukulia hatua za kisheria,”alisema Makachia.

Naye Ofisa Uhusiano wa Shirika hilo Johanes  Emmanuel alisema, kila mzazi anatakiwa  kutoa elimu  ya kupinga  ukatili  dhidi ya watoto sambamba na kukemea vitendo hivyo.

Kwa upande wa Mjumbe wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi  (CCM), wilaya ya Nyamagana Kitati Wambura  na Katibu wa Jumuiya ya Wanawake BAKWATA Mkoa wa Mwanza Bi Sikitu Abubakari walisema,  kuna kila haja ya jumuiya mbalimbali kupiga kelele juu ya ukatili dhidi ya watoto ili kuepuka kuwa na taifa lenye ukatili duniani.

Naye Katibu  Mwenezi wa Chama cha  Demokrasia na Maendeleo Chadema wilaya ya Ilemela  Julius Malifedha alisema, ili kuepusha ukatili ni vema  wanasiasa wakawa na utaratibu wa  kuwakumbusha wananchi juu ya  kukemea vitendo  hivyo.

No comments:

Powered by Blogger.