LIVE STREAM ADS

Header Ads

SHIRIKA LA UNDER THE SAME SUN LAWAFUNDA WENYE UALIBINO.

Na James Salvatory, BMG Dar
Shirika la Kimataifa la Kuetetea watu wenye Ualbino la Under The Same Sun (UTSS), limetoa mafunzo kwa watu 60 wenye ulemavu wa ngozi lengo likiwa ni kuwasaidia kupata ajira mara baadaya kuhitimu masomo yao.

Mafunzo hayo ni pamoja na Sheria Kazi,Sheria ya watu wenye ulemavu na mikataba inayowalinda watu wenye.

Akizungumza na wanahabari Mkurugenzi Mtendaji UTSS, Vicky Ntetema, amesema kuwa mafunzo hayo yana dhaminiwa na Ubalozi wa Canada  nchini Tanzania na Mafunzo hayo yatawanufaisha katika nyanja tofauti ikiwemo jinsi ya kuomba kazi, na kwa upande wa wanaoamua kujiajiri tunawapa nyenzo na mbinu za kuanza biashara.

"Mafunzo haya yanawasaidia vijana hawa kupata ajira na vitu vya kuandaa wakati wa kutafuta ajira hii ni kutokana na watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) hukosa ajira mara nyingi pindi wanapomaliza masomo yao". Alisema Ntetema.

Shega Mboya ni mmoja kati ya Wahitimu hao na ameeleza kuwa changamoto kubwa ni kutopewa nafasi ya kuonyesha uwezo wao mahala pa kazi pindi wanapotuma maombi.
Mkurugenzi Mtendaji UTSS, Vicky Ntetema
Semina ikiendelea

No comments:

Powered by Blogger.