HUDUMA ZA AFYA ZIENDELEE KUBORESHWA NCHINI IKIWEMO HOSPITALI YA WILAYA TARIME MKOANI MARA.
Ahsante kwa Hekima zako Dr.Sammy, Jamii inakutegemea sana, hivyo hitimu vyema masomo yako ili ukaihudumie.
Nasaha za BMG ni kwamba, huduma za afya nchini bado ni Changamoto kubwa nchini kwani katika hospital, zahanati na vituo vya afya ikiwemo hospitali ya Wilaya Tarime upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ni kilio kikubwa. Ukitaka kuelewa, uguliwa/ ugua ndipo utanielewa vyema.
Nina imani Serikali itaendelea kuboresha upatikanaji wa dawa, vitendea kazi pamoja na maslahi ya wahudumu wa afya ili kuwa ari ya kutetea afya za wananchi. Tuwaombee wagonjwa wote (akiwemo mama yangu mzazi) wapate ahueni mapema, Amen". George Binagi wa #LakeFm & #BMGHABARI
No comments: