LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA.

KWAMBA TAREHE 27.11.2016 MAJRA YA SAA SABA (01:00HRS) USIKU KATIKA MTAA WA MAHINA ALLIANCE KATA YA MHANDU WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA RAIA WA MCHINA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA MAIHAIMIYAN MAI @ MINGO, MIAKA 33, MKAZI WA MAHINA, MFANYA BIASHARA WA MABONDO, ALIUAWA KWA KUPINGWA RISASI KIFUANI NA WATU WANAOZANIWA KUWA NI MAJAMABAZI WALIOVAMIA NYUMBANI KWAKE NA KUJERUHI WENGINE WATATU.

INADAIWA KUWA MAJIRA TAJWA HAPO JUU MAREHEMU ALIKUWA ANATOKA KWENYE SHUGHULI ZAKE ZA KIBIASHARA, NDIPO GHAFLA ALIOPOKUWA ANAINGIA KWENYE GETI LA NYUMBANI KWAKE ALIKUTANA NA WATU WATATU WALIOVAMIA NYUMBA YAKE MMOJA KATI YAO AKIIWA NA SILAHA NDIPO ALIMFYATULIA RISASI MOJA ILIYOMLENGA KIFUANI NA KUFARIKI DUNIA.

KATIKA TUKIO HILO MAJAMBAZI HAO WALIMSHAMBULIA PIA MDOGO WA MAREHEMU AITWAYE AYONI MAI MIAKA 29, MCHINA, MFANYABIASHARA WA MABAONDO ALIYEKUWA AKIISHI NAE HAPO NYUMBANI KWAKE KWA KUMPIGA MARUNGU SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KUFANIKIWA KUMPORA FEDHA KIASI CHA SHILINGI LAKI SITA NA SIMU MBILI AINA YA IPHONE, AIDHA WALIMSHAMBULIA PIA KWA MARUNGU MKE WA MDOGO WA MAREHEMU AITWAYE CHRISTINA KINYONGE NA KUMPORA FEDHA KIASI CHA LAKI TANO.

AIDHA MAJAMBAZI HAO WALIMJERUHI PIA KWA RISASI MLINZI WA NYUMBA HIYO ALIYEJULIKANA KWA JINA MOJA LA PASCAL MIAKA 35, KWA KUMPIGA RISASI ILIYOMPARAZA KISOGONI WAKATI AKITAKA KURUKA UKUTA NA KUKIMBIA, MAJERUHI WOTE WATATU WAMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO WAKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU, MWILI WA MAREHE UMEHIFADHIWA  HOSPITALI YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI. JESHI LA POLISI LINAWASAKA WATUHUMIWA WOTE WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI AUGUSTINO SENGA ANATOA WITO KWA WAKAZI WA  JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI JUU TAARIFA ZA WAHALIFU HAO ILI WAWEZWE KUKAMTWA  NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA, ALIONGEZA KUWA WANANCHI WASIWE NA MASHAKA WAWE WATULIVU ILI JESHI LA POLISI LIWEZE KUTENDA KAZI IPASAVYO.

KATIKA TUKIO LA PILI MNAMO TAREHE 26.11.2016 MAJIRA  YA SAA 15:35HRS KATIKA KIJIJI CHA LUHAMA KATA YA BANGWE WILAYA YA SENGERMA JIJI NA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKIWA DORIA NA MISAKO WALIFANIKIWA KUWAKAMTA WATU WATANO KWA TUHUMA ZA KUKUTWA WAKIWA NA NYAVU HARAMU 40  ZA AINA YA TIMBA WANAZOZITUMIA KATIKA SHUGHULI ZA UVUVI.

WATUHUMIWA WALIOKAMATWA WALIJULIKANA KWA MAJINA YA 1. KADOSI KAYOKA MIAKA 45, 2. JAPHET CLEMENT MIAKA 29, 3. IMANI WILSONI MIAKA 20, 4. ELIA KATOKA MIAKA 35, NA 5. MACHUMU KULINGWA MIAKA 81, WOTE WAVUVI WA KIJIJI CHA LUHAMA. ASKARI WALIFANIKIWA KUWAKATA WATUHUMIWA TAJWA HAPO JUU BAADA YA KUPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA JUU YA UWEPO WA WATU WANAOJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU, NDIPO ASKARI WALIFIKA ENEO LA TUKIO NA KUFANIKIWA KUWATIA NGUVUNI.

JESHI LA POLISI LIPO KATIKA MAHOJIANO NA WATUHUMIWA WOTE, AIDHA UPELELEZI NA MSAKO WA KUWASAKA WATU WENGINE WANAOJIHUSISHA NA UHALIFU HUO  BADO UNAENDELEA.

PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATUHUMIWA WOTE WATAFIKISHWA MAHAKAMANI ILI HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA DHIDI YAO.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI AUGUSTINO SENGA ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA WAACHE KUJIHUSISHA NA SHUGHULI ZISIZO HALALI, ALIONGEZA KUWA JESHI LA POLISI LINAWAOMBA WANANCHI WAENDELEE KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LAO ILI LIWEZE KUDHIBITI UHALIFU KATIKA MKOA  WA MWANZA.

IMETOLEWA NA: ACP: AUGUSTINO SENGA KAIMU KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

No comments:

Powered by Blogger.