LIVE STREAM ADS

Header Ads

KABAGO, MKONGWE KWENYE MUZIKI WA KUCHANA NCHINI KUACHIA WIMBO MPYA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Kupitia redio mbalimbali nchini pamoja na mitandao ya kijamii, kesho jumatano Novemba 09, 2016 msanii mkongwe wa muziki wa kuchana, Filbert Kabago "Kabago", ataachia wimbo wake mpya uitwao Tanzania akiwa amemshirikisha mkongwe mwenzake Hadmad.

Kabago anatambulika kama mmoja wa watu waliowezesha hiphop nchini kusonga mbele tangu akiwa mkoani Arusha na hata alipohamia Mwanza, akiwa kama msanii na mtangazaji wa redio (kwa sasa Passion Fm Mwanza).

Atakumbukwa namna alivyosaidia kwenye harakati za kimaendeleo Jijini Mwanza kupitia kazi zake za muziki na hata namna wimbo wa tatizo la umeme ulivyoleta nafuu kwa wakazi wa Jiji la Mwanza.

Kama hiyo haitoshi, mchango wake redioni ni mkubwa kwa wasanii mbalimbali hususani wanaochipukia ambapo wengi wao ambao sasa ni wanavuma akiwemo Baraka Da Prince na Young Killer, wamepitia mikononi mwake. 

Kupitia BMG, kaa tayari kuusubiri wimbo wa Kabago uitwao Tanzania ambao umetengenezwa kwenye studio yake iitwayo K-Records chini ya produza Sam Music.

No comments:

Powered by Blogger.