Mkuu wa Wilaya ya Tarime aanza kutumbua vinara wa rushwa katika mpaka Tanzania na Kenya wa Sirari.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Tarime(DC) Glorious Luoga ameaanza kutumbua maafisa ambao wanatuhumiwa kuwa vinara wa rushwa katika mpaka wa Sirari.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake jana, DC Luoga aliagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru kumchunguza mmoja wa maafisa wa TRA katika mpaka huo wa Sirari kwa tuhuma za kupokea rushwa ya sh milioni 15 kupitia akaunti ya mdogo wake kwa lengo la kumsadia mmoja wafanyabiashara ambaye alitakiwa kulipa kodi sh milioni 48 na badala yake akalipa kodi ya Shilingi milioni 23.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya ameshauri kamishina wa TRA kumchukulia hatua afisa huyo(jina tunalo) wakati uchunguzi ukiendelea na kutoa onyo kali kwa watumishi wengine kuepukana na vitendo vya rushwa ili waweze kusadia serikali kufikia lengo la kukusanya mapato kwa maendeleo ya taifa.
Imeandaliwa na Mtandao wa Mara Online

No comments: