LIVE STREAM ADS

Header Ads

UJENZI CHINI YA KIWANGO WAUA WATU WAWILI JIJINI MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na Conges Mramba
Wakazi wawili wa Jijini Mwanza, Twalib Nassib (18) na mwenzake, Yusuph Masunga (32)ambao walikuwa vibarua wa ujenzi, wamefariki dunia katika ajali ya kuangukiwa na kanopi ya jengo la ghorofa moja wakati wakiendelea na shughuli za ujenzi.

Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi,Ahmed Msangi, amesema jijini hapa kwamba juzi Novemba 6, majira ya saa 11:30 jioni katika eneo la mtaa wa Buganda, kata ya Mkolani wilaya ya Nyamagana, jijini Mwanza, watu hao walifariki kufuatia ajali hiyo.

Inadaiwa kuwa vibarua hao wote ni wakazi wa jijini humo walikuwa wamepewa kibarua cha kuzibua mtaro uliopo pembeni mwa jengo hilo na mmiliki wa jengo aiwaye, Gaston David maarufu kwa jina la Ikoko (56), ndipo ghafla ajali hiyo ilitokea na kuwasababishia wote wawili kupoteza maisha.

Jeshi la polisi linamshikilia mmliki wa jengo hilo, kwa mahojiano zaidi, aidha uchunguzi wa awali umebainisha chanzo cha ajali ni ujenzi wa jengo uliokuwa chini ya kiwango.

Kamanda Msangi amesema miili ya marehemu wote wawili imehifadhiwa hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa ajili ya uchunguzi.
Bonyeza HAPA Kwa taarifa zaidi

No comments:

Powered by Blogger.