LIVE STREAM ADS

Header Ads

NASAHA ZA BMG KUHUSU UWANJA WA NYAMAGANA JIJINI MWANZA.

Huu ni mwonekano wa Uwanja mkongwe wa Nyamagana Jijini Mwanza baada ya kuwekewa nyasi bandia. Uko kwenye hatua za mwisho kukamilika licha ya kupitia figisufigisu nyingi ikiwemo nyasi kukwamba bandarini kwa muda kwa kisingizio cha TFF kushindwa kulipa kodi ya nyasi hizo.

BMG inasema "Ahsante kwa walionusuru hilo. Lakini pia walionusuru kuuzwa kwa uwanja huu ili ijengwe hoteli utadhani Mwanza kuna uhaba wa maeneo ya uwekezaji. Aibu!".

Licha ya kuwa na historia pana kwenye masuala ya kijamii na ukombozi wa Tanganyika, kwenye soka itakumbukwa kwamba mwaka 1974 timu za Simba na Yanga zilikutana kwenye uwanja huu kwenye Fainali ya Ligi ya Taifa ya Soka ambapo Yanga iliichapa Simba bao 2-1.

BMG tunahimiza kwamba, pamoja na wadau wengine, Kampuni ya Mafuta ya MOIL kama ilivyoahidi kupitia kwa Mkurugenzi wake, Altaf Mansoor, ipewe fursa ya kutekeleza ahadi yake ya ujenzi wa majukwaa kwenye uwanja huu mkongwe tangu mwaka 1945 ili sasa uwe na hadi yake.
'\
BMG inatamatisha nasaha zake kwa kushauri ipigwe mechi ya Simba na Yanga hata kama ni ya kirafiki kwenye ufunguzi wa uwanja huu na mechi hiyo itanguliwe na visiki vya Mwanza ambavyo ni Toto, Pamba, Mbao na Alliance.
BONYEZA HAPA KUTAZAMA PICHA

No comments:

Powered by Blogger.