LIVE STREAM ADS

Header Ads

ONGEZEKO KUBWA LA IDADI YA WATU NCHINI LAITISHA SERIKALI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvatory, BMG Dar
Serikali imesema ongezeko kubwa la watu kila mwaka  ni changamoto kubwa nchini hali ambayo inasababisha sekta ya afya kuonekana haina maboresha ya kutosha kila mwaka

Naibu Waziri wa afya, jinsia, wazee na watoto, Dkt.Khamisi  Kingwangala, alisema kuongezeka kwa  watoto milioni moja  kwa kila mwaka kunasababisha hadi kufikia miaka 50 ijayo Tanzania kuwa na zaidi ya watu milion 100 hali ambayo itasababisha sekta hiyo kuwa na changamoto kubwa.

Aliyasema hayo jana katika kuadhimisha miaka 50 ya ushirikiano na, Ubalozi wa Uswisi nchini ambapo  kumefanyika mdahalo wa kujadili hali ya upatikanaji wa huduma bora za afya nchini, mdahalo ambao umehusisha viongozi wa Tanzania na Uswisi lakini pia kushirikisha watu kutoka mashirika binafsi.

Aidha kingwangala amesema serikali imejipanga  kuweka  utaratibu wa kila mwananchi kuwa na bima ya afya japo  kuwa kuna tatizo kubwa Kwa magonjwa yaliyopewa msamaha wa kutibiwa bure.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya ukimwi na mbunge wa kigamboni Dkt. Faustane Ndugulile, alisema ni vyema vijana na wananchi kupewa elimu ya kutosha kuhusu uzazi wa mpango ili kuweza kuthibiti ongezeko hili la idadi ya watu 

Mdahalo huo ulifanyika ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 50 ya ushirikiano baina ya Tanzania na Uswisi na katika mdahalo huo mambo mbalimbali yanayohusu sekta ya afya yalijadiliwa ikiwa ni pamoja na utoaji wa huduma, miundombinu, fedha, madawa na vifaa tiba.

No comments:

Powered by Blogger.