LIVE STREAM ADS

Header Ads

WASANII MKOANI MWANZA WATAKIWA KUSAIDIA UTOKOMEZAJI WA UKATILI WA WATOTO MAJUMBANI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Wasanii mbalimbali mkoani Mwanza wakiwemo wa maigizo na muziki wametakiwa kutunga nyimbo na filami zenye kuelimisha  jamii juu ya kupinga ukatili  wa watoto majumbani pamoja na kutetea haki za watoto hao.

Hayo yalisemwa juzi kwenye mafunzo ya kupinga ukatili majumbani na Ofisa  Uelimishaji  wa  Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na  kupinga ukatili majumbani  Foundation Karibu Tanzania (FKT)Erick Karongo,yaliyofanyika kwenye uwanja wa shirika hilo,lililopo wilayani Ilemela mkoani hapa.

Alisema  kila msanii anatakiwa kukemea vitendo hivyo kupitia  kazi zao za sanaa, ikiwemo nyimbo,maigizo,shairi na ngonjera za kuelimisha jamii dhidi ya ukatili

Pia alisema,  lazima mzazi  atambue umuhimu wa  mtoto  kwa kumthamini na kumpenda kwani  kufanya hivyo kutapunguza  ukatili  kwa watoto.

Naye  Mkurugenzi  kikundi cha Hangano Cultulral Troupe, Peter Haule, alisema, kupitia mafunzo hayo  wataelimisha jamii kwa njia ya sanaa ili kupinga ukatili kwa watoto.

“Tunalishukuru  shirika hili kwa kutoa mafunzo haya, kwani tukiwa kwenye matamasha tutatunga nyimbo za kuelimisha jamii juu ya ukatili wa watoto majumbani kwani  kumfanyia  vitendo hivyo ni  kumnyima haki yake na kinyume na sheria," alisema Haule.

 Kwa upande wa Ofisa Uhusiano Johanes Emmanuel,alisema  kuvunja ukimya  kutasaidia  kupunguza watoto wa mitaani  kwani lengo la kuanzisha kituo hicho ni kutetea   watoto wanaofanyiwa vitendo vya kikatili.

No comments:

Powered by Blogger.