LIVE STREAM ADS

Header Ads

UJUMBE KUTOKA CHAMA CHA CPC CHA CHINA WATUA NCHINI KUJIFUNZA KAZI ZA CCM.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Madabida (kushoto), akimkabidhi Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015,  Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano ya Kimataifa, Maendeleo na Mafunzo wa Chuo cha Viongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, Jia Bo,  Dar es Salaam leo asubuhi, ambaye yupo nchini na wajumbe wenzake sita kwa zaiara ya siku saba ya kichama kukitembelea Chama Cha Mapinduzi (CCM).
 Mkutano ukiendelea.
 Wajumbe hao wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida.
 Makada wa CCM wakijumuika na wajumbe wenzao kutoka china.
 Mratibu wa Masuala ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Pindi Chana (kushoto), akizungumza na wajumbe hao.
 Madabida akiwakaribisha wajumbe hao.
Karibuni wajumbe kutoka China.


Na Dotto Mwaibale
UJUMBE wa watu sita kutoka Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) umewasili nchini kwa ziara ya siku saba kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Madabida alisema ujumbe huo umeongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano ya Kimataifa, Maendeleo na Mafunzo wa Chuo cha Viongozi wa chama hicho, Jia Bo.

Madabida alisema ziara ya ujumbe huo hapa nchini ni kudumisha ushirikiano baina ya Tanzania na China ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa na kiongozi wa Taifa hilo Hayati Mao  Tse-Tung.

Alisema ujumbe huo ambao utatembelea Wilaya ya Temeke na Zanzibar umewasili nchini kufuatia ziara ya baadhi ya makada wa CCM walipokwenda nchini China ambapo walijifunza mambo mbalimbali ambayo ujumbe huo utapenda kujua kama wameyafanyia kazi.

Mratibu wa Masuala ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Pindi Chana alisema ujio wa viongozi wa chama hicho kutoka China ni matunda ya ushirikiano wa Tanzania na nchi mbalimbali duniani.

" Ujio wa wenzetu hawa kutoka China ni matunda ya ushirikiano kati yetu na nchi nyingine kama Zimbabwe, Afrika Kusini, Angola, Cuba,  Ulaya hasa katika siasa za kijamaa" alisema Chana.

Alisema wenzetu wa China wapo karibu bilioni moja na wamepiga hatua katika maeneo mbalimbali hivyo ujio wao hapa nchini ni fursa kwao kujifunza mambo yetu na sisi kujifunza kwao kutokana na hatua ya kiuchumi waliyonayo.

No comments:

Powered by Blogger.