LIVE STREAM ADS

Header Ads

SHIRIKISHO LA VYUO VIKUU NCHINI LATAKA SERIKALI KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA MIKOPO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvatory, BMG Dar
Shirikisho la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu Tanzania limetoa siku saba kwa serikali kushughulia changamoto mbalimbali zinazowakabili wanafunzi kuhusu mikopo.

Akizungumza  na wandishi wa habari Jijini dar es salaam  katibu msaidizi wa shirikisho hilo, Daniel Zenda amezitaja baadhi ya hujuma ambazo anadai zinafanywa kwa makusudi na watendaji kutoka bodi ya mikopo ili kumkwamisha Rais John Magufuli.

Aidha amesema wanasikitishwa  juu ya hujuma zinazoendelea kule bodi ya mikopo na wamehuzunishwa kwa kiwango kikubwa baada ya sakata hili la mikopo kuchukua taswira mpya ndani ya nchi, ambayo haipendezeshi sekta ya elimu, kwa hiyo wamemejiridhisha kuwa kuna hujuma zinafanyika dhidi ya serikali ili kumkwamisha Rais Magufuli.

"Miongozo kutoka bodi ya ya mikopo na mwingine kutoka Wizara ya Elimu, hii miongozo inakinzana, athari ya kupingana kwa hii miongozo inapelekea wanafunzi wengi kukosa mikopo, kigezo cha umri hakipo katika miongozo yote miwili lakini kule bodi ya mikopo kinatumika sisi tunaona ni hujuma mojawapo," alisema

No comments:

Powered by Blogger.