LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAZIRI WA ELIMU ATOA NENO KWA VIJANA NCHINI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Displaying IMG_20161122_094945.jpgNa James Salvatory, BMG Dar
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, amewataka Wadau wa Sekta ya Elimu nchini kuwakumbusha vijana kuzingatia maadili na kuondokana na vitendo vya rushwa ili kujenga jamii yenye bora nchini.

Akizungumza katika Mdahalo wa kukuza nakujenga maadili jijini Dar es Salaam, Waziri Ndalichako alisema kuwa kumekuwa na baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwatetea watoto wao pindi wa napokutwa nauvunjifu wamaadili hali inayochangia kuwepo kwa kiwango kikubwa cha mmongo'nyoko wa madili  kwa vijana.

Waziri Ndalichako alisema kuwa Suala la Maadili nisuala Muhimu katika Makuzi ya Vijana ambayo inanalenga kumtambulisha mtu kwenye jamii yake nakuwa kielelezo muhimu chakupima Maadili ndani jamii na Msingi Mkubwa wa Maadili unajengwa ndani ya familia ambapo baadhi ya vijana wanatokea katika familia hizo nakuwataka wavijana hao kuweza kuiga matendo mema na kuepuka vitendo viovu.

''Mnatakiwa kuzingatia matendo Mema  epukeni Matendo Maovu na hakikisheni muda wote mnakuwa wasikivu na mnaofundishika ''alisema Ndalichako.

Katika hatua Nyingine Mkurugenzi wa Taasisi ya kudhibiti na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU ) Vallentino Mlowa amesema kuwa ili jamii iweze kuwa na maadili  ielimishwe juu ya umuhimu yakuwa  na maadili mema katika jamii.

Mlowa Alisema kuwa nivyema Wizara nataasisi hiyo kukuweza kukaa pamoja ilkuweza kujenga mitaala itakayo jenga jamii iliyo bora .

No comments:

Powered by Blogger.