LIVE STREAM ADS

Header Ads

SHIRIKA LA HAKI ELIMU LAIHEUKIA SERIKALI, LATAKA KIUNDWE CHOMBO CHA JUU CHA ELIMU.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Displaying IMG_20161121_103703.jpgNa James Salvatory, BMG Dar
Baada ya serikali kuyarudisha mafunzo ya ualimu chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi,Teknolojia na Ufundi, Shirika lisilo la Kiserikali la Haki elimu limeitaka serikali kuunda chombo chenye mamlaka ya juu katika elimu yaan (Education Regulatory  Authority ) chini ya sheria ya elimu ili kusimamia na kulinda sera, sheria, kanuni na miongozo ya elimu iliyowekwa ili kupunguza maamuazi na mambadiliko ya mara kwa mara katika sekta  ya elimu nchini.

Hayo yalisemwa Jiji Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa haki  elimu, John Kalage   wakati akizungumza na wanahabari ambapo alibainisha kwamba inaonekana waziri wa elimu ana mamlaka makubwa ya kutoa maamuzi hali inayosababisha kuwepo na nyaraka nyingi za elimu  zinazobadilika kila mara  hata kabla ya kufanyiwa kazi kikamilifu na kutakiwa kuundwa kwa chombo chenye mamlaka kama ilivyo bodi ya  uhasibu ( NBAA) ambayo inaratibu taaluma ya uhasibu nchini kote .

"Kama Taifa tunapaswa kuwa na dira ya elimu isiyotegemea matakwa ya mtu mmoja hata kama ni waziri, haiwezekani kila waziri akiteuliwa anakuja kutekeleza mipango yake inavyoathiri mamilioni ya vijana kadiri atakavyo bila jamii kwanza kupata fursa ya kuijadili".Alibainisha na kuongeza;

"Kwanza mabadiliko ya mara kwa Mara katika mfumo  wa elimu yetu yanaashiria kutokuwepo na mipango endelevu ya elimu , pia ni dalili ya kukosa umakini katika masuala yenye maslahi ya nchi".Alisema.

Aidha Kalange  alipongeza serika kwa maamuzi ya kuyarudisha mafunzo ya ualimu chini ya wizara ya elimu na Kusisitiza kuwa ni vyema mafunzo ya ualimu ngazi zote yakaendelea kutolewa tu na vyuo vikuu  na vyuo vya ualimu peke yake na serikali kuharakisha uundaji wa bodi ya kitaalamu ya waalimu.

"Pamoja  na mambo mengine bodi hii itasaidia kuweka na kibaini viwango bora vya kitaaluma ya ualimu pamoja na kusimamia maslahi yao hivyo kusaidia kuboresha ubora wa walimu na elimu nchini" Aliongeza kalange

No comments:

Powered by Blogger.