LIVE STREAM ADS

Header Ads

CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOANI MARA CHATANGAZA MKAKATI KABAMBE 2017.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Mara (MRPC), Mugini Jacob, akitangaza mikakati ya Chama hicho.
Na MRPC
Viongzi wa MRPC
Kamati tendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara(MRPC), itaanza kutumia teknolojia ya mtandao wa internet kufanya vikao vyake mara kwa mara ili kuongeza ufanisi wa kazi na kupunguza matumizi yasio ya lazima.

Mwenyekiti wa MRPC, Mugini Jacob, alitangaza mpango huo jana katika Mkutano Mkuu wa MRPC (Annual General Meeting 2016) uliofanyika katika bwalo la jeshi la polisi mjini Musoma.

Jacob alisema MRPC imeendelea kuimarika na kuwa na mahusiano mazuri na wadau ndani na nje ya Mkoa na kuonya kuwa mwanachama yeyote atakaye jaribu kurudisha maendeleo ya chama nyuma au kuharibu mahusiano hayo kwa kujihusisha na vitendo vya kukiuka maadili ataondolewa kwenye chama mara moja.

No comments:

Powered by Blogger.