LIVE STREAM ADS

Header Ads

JICHO LA BMG KATIKA BARABARA YA MWANZA-MUSOMA.

Ukiwa unatoka au kwenda Mwanza, barabara ya Musoma, kilomita chache kutoka mji wa Magu, kuna daraja la vyuma, inasemekana lilijengwa na wanajeshi miaka mingi iliyopita.

Hilo daraja naamini bado ni imara, ila kiuhalisia halistahili kuwepo miaka hii kwani inawalazimu madereva kusubiriana, magari mawili hata madogo hayapishani.

Ni vyema serikali ikalifanyia kazi suala hili maana ni barabara kuu tena tegemeo kwa mabasi ya abiria na mizigo kutoka ndani na nje ya nchi jirani ya Kenya kama si ya wale waendao/watokao kwa Baba wa Taifa, Julius Kambarage Nyerere (mkoani Mara).
Ahsanteni kwa kuwa nasi.
BMGHabari

No comments:

Powered by Blogger.