LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC KINONDONI AHIMIZA WAKALA WA MISITU KUSAIDIA MBAO ZA UJENZI WA MADARASA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com


Na James Salvatory, BMG Dar
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es salaam, Ally Hapi, ameiomba  Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kuwasaidia mbao kwa lengo la  ujenzi wa vyumba vya  madarasa .  

Akizungumza leo katika hafla fupi ya kukabiziwa madawati  80 yenye thamani ya shililingi milioni tano na laki sita kutoka kwa  wakala wa huduma za misitu  Tanzania  mkuu  huyo wa wilaya  amesema  kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi  kwa sasa, wanaupungufu wa vyumba vya madarasa  1,068, na upungufu wa matundu ya vyoo  2,759 ,katika shule za msingi katika manispaa ya kinondondoni .

Aidha hapi amesema kuwa  Raisi wa jamuhuri wa muungano wa Tanzania  John Pombe Magufuli  aliwasaidi fedha za kujenga madarasa 22 na kwa fedha hizo wameshajenga shule mbili mpya na kuna wadau mbalimbali wameshawaidia vifaa mbalimbali vya ujenzi ikiwemo mabati,simenti na kuwaomba mbao ambazo zitaweza kujenga vyumba 1068 na kuwaomba wadau wengine wote waweze kuunga juhudi za ujenzi wa vyumba vya madarasa na vyoo vinavyoikabili wilaya ya kinondoni

Naye meneja wa wakala wa huduma za misitu Tanzania Alexander Mboya amekabizi madawati  80 yenye thamani ya shililingi milioni 5  na laki sita kwa ajiri ya shule za msingi mbili ikwemo ya msingi kigogo na Ilonda ambayo kila shule itapata madawati 40.

No comments:

Powered by Blogger.