LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM ATIMIZA AHADI ZAKE KWA WAKATI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvatory, BMG Dar
Mkuu wa mkoa wa Dar es saalam, Paulo Makonda, leo amekabidhi  vitu mbalimbali  vyenye thamani ya shilingi milioni 164  ikiwa ni  ahadi zake kwenye ziara alizofanya mwezi Novemba mwaka huu katika mkoa huo.

Akikabidhi vitu hivyo, amewaahidi waathirika wa madawa ya kulevya ambao wako nyumba za utimamu (Soba Souses), watendaji waliofanya vizuri katika shughuli  za maendeleo  kwa kuwapa pikipiki, kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) kwa kutoa zawadi ya gari, mama aliyepewa laki mbili kwa ajiri ya mtaji pamoja na  kijana aliyepewa milioni moja kwa ajiri ya mtaji wa biashara

Aidha Makonda amekabidhi zawadi ya mabati  2000 kwa ajiri ya sekondari ya Jitegemee na shule ya msingi Annex Mbagala  mabati 1000 na shule ya Katoliki kupewa simenti 1000,ametoa tumba  kwa ajiri ya bendi ya jeshi.

Kwa upande wao waliopatiwa zawadi hizo kwa ujumla wao wamepongeza juhudi za mkuu huyo wa mkoa kwani ahadio nyingi alizotoa ameweza kuzimiza kabla hata ya mwaka kuisha.

No comments:

Powered by Blogger.