KUHUSIANA NA SAKATA LA MACHINGA JIJINI MWANZA.
Nimeguswa na suala hili, hapa kuna pande mbili zinazohusika, moja ni Serikali kwenye kusimamia agizo lake na pili ni kwa wanachinga wanaoomba hurma ya Serikali ili waendeleee kuwepo.
Ni wazi Serikali ina dhamira nzuri ya kusimamia sheria zake kwenye halmashauri hasa kwenye kuliweka Jii safi na kulinda maslahi ya wale wanaofanya biashara kihalali baada ya kulasimisha biashara zako (business formalization)
Sheria hizo ni muhimu sana na zinatumika katika Majiji mbalimbali kama Nairobi, Kampala na kwingineko, nina imani Serikali ya Mkoa wa Mwanza wanatumia mode hiyo kwa nia njema.
Madai ya wanachinga nayo yana msingi wake kuwa, wangeandaliwa maeneo mengine hapa Mjini kwa ajili ya biashara , nukuu ya kauli ya Rais inatumiwa sana, kwa wao kuona wanaendelea kufanya biashara kwenye maeneo ya mijini.
Kimsingi kuna kila sababu ya kuathirika kiuchumi endapo wataenda katika maeneo ambayo serikali imewapangia kwani hayajafanyiwa upembuzi wa awali kwenye kubaini manufaa/hasara za maeneo hayo, ndio maana wengi wamekuwa wanyenyekevu wakiiomba serikali kufikiria upya uamuzi huo.
Mtazamo wangu
Suala la maridhiano ndilo pekee linaloweza kusaidia kumaliza mgogoro huu, kuliko njia nyingine yoyote ile, serikali ikubali kupoteza sehemu ya maamuzi yake (Mandatory decision) na wamachinga wakubali kupoteza nusu ya maslahi yao (Win – win situation).
Suala la maridhiano ndilo pekee linaloweza kusaidia kumaliza mgogoro huu, kuliko njia nyingine yoyote ile, serikali ikubali kupoteza sehemu ya maamuzi yake (Mandatory decision) na wamachinga wakubali kupoteza nusu ya maslahi yao (Win – win situation).
Najua serikali ina nia njema sana kwenye hili lakini ni vyema ikajaribu kutazama na utetezi wa upande wa pili ili iweze kujenga mahusiano mazuri na wananchi wake, ambao pia ni wapiga kura kwenye uchaguzi ujao wa mwaka 2020
Ebu tuone hili kwa jicho la fundi saa (smart thinking), na ikumbukwe kuwa, Rais wetu ni mtu wa wananchi wa kawaida kwani kwa kauli yake ndio waliomchagua.
Nakumbuka wimbo ule wa Tanzania kisiwa cha amani nahisi tutaukumbuka, sidhani kama matumizi ya nguvu yatasaidia kumaliza mgogoro huu.
Namjua mkuu wa Mkoa wa Mwanza kaka yangu John Mongella ni mtu mwenye uwezo mkubwa ana kila sababu ya kutumia vipawa vyake kwenye kuliona jambo hili.
“Hivi tunashindwaje kufunga barabara moja na tukawaruhusu watu wetu wakafanya biashara na tukakusanya kodi” Alisema Mh. Rais kwenye ziara yake ya kuwashukuru wakazi za Mwanza kwa kumchagua, ipo mifano mingi inayotumiwa na miji mbalimbali lakini kwa misingi ya kutazama faida na hasara ya jambo ( cost-benefit analysis).
Aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela aliamini maridhiano ndio msingi mkubwa wa mgogoro wowote ule.
Edwin Soko, Mwanahabari
Edwin Soko, Mwanahabari
No comments: