LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AKAGUA UJENZI WA OFISI MPYA ZA BAKWATA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvatory, BMG Dar
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, leo amefanya ziara kwenye ofisi za Baraza Kuu la Waislamu nchini (BAKWATA) na kukagua ujenzi wa jengo jipya la ofisi za baraza hilo.

Injia wa taasisi ya GSM Foundation inayofadhili ujenzi huo, Hersi Said, ameeleza ujenzi huo uko katika hatua nzuri na kwamba ghorofa ya kwanza imekamilika na kuhaidi kuw wiki mbili zijazo ghorofa ya pili itakuwa tayari ambapo unataraji kukamilika mwezi june mwakani.

Amebainisha kwamba jengo hilo litakuwa na Ukumbi wa Mikutano, Maktaba, Kompyuta,lifti, ofisi za kisasa za Mufti zikiwa nne katika ghorofa ya tatu na ofisi nyingine ya Sheikh Mkuu wa Mkoa, Katibu Mkuu wa BAKWATA, Kadhi, Baraza la Maulamaa, kumbi za wanawake na Studio.

Naye RC Makonda amesisitiza juu ya ujenzi huo kukamilika kwa wakati ili ifikapo mwezi mtukufu wa Ramadhani hapo mwakani, ofisi hizo ziweze kutumika.

Muft Mkuu wa Tanzania, Aboubakari Zubeir, ameishukuru taasisi ya GSM Foundation na Serikali kwa kufanikisha ujenzi wa jengo hilo na kuwataka waumini wa dini ya kiislamu kote nchini kuwaombea viongozi wa Serikali ya awamu ya tano akiwemo Rais John Magufuli katika utendaji wao wa kazi kwa watanzania wote.

No comments:

Powered by Blogger.