LIVE STREAM ADS

Header Ads

MADALALI WA BIMA NCHINI WAPIGWA MSASA JIJINI DAR ES SALAAM.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

 NaJames Salvatory BMG-Dar
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa mafunzo ya siku moja kwa Madalali wa Bima Tanzania yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kuifahamu vema Sheria ya Kodi ya Mwaka 2014 ili waweze kushiriki vema katika ulipaji wa kodi ya ongezeko la thamani kutoka sekta ya Bima.

Akizungumza jana Jijini Dar es salaam, Meneja wa Elimu kwa Mlipa Kodi wa (TRA) Diana Masalla, alisema mafunzo hayo yamewaelimisha wanachama hao juu ya kodi ya zuio, utoaji wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na jinsi ya kulipa kwa njia ya mtandao (Revenue gateway system).

Alisema TRA imekuwa ikitoa mafunzo hayo kwa wanachama na mawakala wa Bima kwa sababu kabla ya sheria ya mwaka 2014 walikuwa hawalipi kodi hivyo semina hiyo imesaidia wanachama hao kuwa na uelewa mpana juu ya ulipajji wa kodi ya ongezeko la thamani VAT.

Mwenyekiti wa Chama cha Madalali wa Bima Tanzania, Mohamed Jaffer, aliipongeza TRA kwa hatua ya kutoa elimu kwa wanachama wake kwani imesaidia kuwajengea uwezo ambao utasaidia ulipaji wa kodi ya ongezeko la thamani VAT.

No comments:

Powered by Blogger.