MAHAFALI YA CHUO CHA UHASIBU JIJINI DAR ES SALAAM YAFANYA.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com









Mgeni rasmi kwenye Mahafali ya Chuo cha Uhasibu nchini, TIA Dar es salaam, Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania Dk.Natu Mwamba, akisikiliza risala kutoka kwa mkuu wa mafunzo wa chuo hicho alipokuwa akielezea kuhusu idadi ya wahitimu na changamoto zinazoikabili taasisis hiyo.
Aliiomba Serikali kuendelea kusaidia kadri ya uwezo wake ili taasisi hiyo iweze kufikia malengo ya kutoa mafunzo ngazi ya shada ya uzamili (Masters). Mahafali hayo yalifanyika jana.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Dk.Joseph Kihanda (katikati akiskiliza kwa makoni Brass Band ambapo yeye kama mkuu wa Taasisi ameelezea Mengi aliyoyafanya kwa Muda mfupi aliokaa katika Taasisis hiyo ikiwemo kutoa Fursa kwa wafanyakazi wengi zaidi kujiendeleza kimasomo hasa ngazi ya Masters na PHD Ambapo hadi sasa waalimu wapatao 12 wanasoma PHD katika hatua mbalimbali,Amejitahidi kuboresha Miundombinu ikiwemo Madarasa ya Kisasa na Ujenzi wa jengo jipya la Ghorofa 6 litakalokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zadi ya 3,000 kwa mara moja na mengine mengi.

Baadhi ya wafanyakazi wakiongozwa na Afisa Habari wa Taasisi hiyo Bi.Lilia Rugaitika wakifuatilia kwa umakini Tukio hilo

Waadhiri Mbalimbali Akiwemo Mr Msabi,Dk.Aniceth Mpanju ,Mr Justin ,Mr Marobe na Mr Bajjet nao wakiskiliza kwa umakini wakati mahafali yakiendelea

Wahitimu mbalimbali wakifuatilia kwa umakini

Wahitimu wa Shahada ya Ugavi na Manunuzi (BPLM )Bwana Hazrat Mandamo akifurahia jambo na Bi. Rosalia Kisongo wakifurahia kwa pamoja baada ya jana kuhitimu


Mhitimu wa Shahada ya Ugavi na Manunuzi (BPLM ) Bi. Radia akifurahia kwa pamoja na wenzake wa Shahada ya Uhasibu (BAC) baada ya Kuhitimu jana

ANGALIA HII VIDEO WAKICHEZA MZIKI KWA PAMOJA KWA FURAHA,WIMBO WA DARASA UNAOITWA MUZIKI
No comments: