LIVE STREAM ADS

Header Ads

+MAONI: RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU NIMR.

Rais Magufuli amteua profesa Yunus Mgaya kuwa mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Taifa ya magonjwa ya binadamu NIMR, akichukua nafasi ya Dkt.Mwele Malecela baada ya uteuzi wake kutenguliwa jana.

MAONI.
Prof. Yunus Mgaya ameteuliwa kuwa mkurugenzi wa NIMR kuchukua nafasi ya Dr Mwele Malecela aliyetumbuliwa jana baada sakata la 'ZIKA'...,

BAADA YA UTEUZI HUO, nimepata mshtuko mkubwa na kujiuliza swali hili..., "kweli Profesa Yunus Mgaya aongoze NIMR?" 
Mtaalam wa 'Animal science'; aquaculture (The cultivation of aquatic produce such as aquatic plants, fish, and other aquatic animals.); na pia fisheries Mbona haziendani na NIMR (utafiti wa magonjwa ya binadamu)?

Unamtoa mtaalam wa 'PARASITOLOGY' (A study of parasites.) unamleta mtu wa mambo ya fisheries, mbobezi wa 'AQUACULTURE' kwenye utafiti wa magonjwa ya binadamu...., kwenye taasisi ya taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR).., how!? 

Anyway; ndivyo tulivyo, hata waziri wa Afya ni mtaalam na mbobezi wa sheria (mwanasheria)..., 

Kila la heri Prof. Yunus Mgaya, nakumbuka alisema bwana mkubwa, atakukumbuka na atakutafutia kazi nyingine.., baada ya ile ya UDSM.., Jifunze kunyamaza huko ulipo (ushauri wangu huo)! 
Martin Maranja Masese (MMM)

No comments:

Powered by Blogger.