LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAONI BAADA YA RAIS MAGUFULI KUTENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU WA NIMR.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli, jana usiku Disemba 16, 2016 ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dkt.Mwele Malecela.

Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa NIMR atakayejaza nafasi iliyoachwa wazi na Dkt.Malecela utatangazwa hapo baadaye.
Disemba juzi 15,2016 Dkt.Mwele alinukuliwa na vyombo vya habari akizungumza kuhusu uwepo wa ugonjwa wa ZIKA Tanzania na kwamba asilimia 15 ya waliopimwa walikutwa na virusi vya ugonjwa huo ambapo hata hivyo taarifa hizo zilikanushwa na wizara ya afya jana.

Maoni Mtandaoni
Ikiwa ni ndani ya siku nne tu tangu niandike na kuhoji kuwa; je,kuna haja ya sisi wanainchi kuendelea kukubali habari tutakazo elezwa na viongozi wetu Mawaziri,wakuu wa taasisi mbali mbali bila ya uthibitisho kutoka Ikulu?.

Hii ilitokana na kadhia ya machafuko hewa juu ya mwekezaji Dangote,baada ya ndugu Mh:Muhongo na Mh: Mwijage kunukuliwa wakisema; Dangote alitaka Gesi ya bure then auziwe makaa ya mawe kwa bei chee huku shirika la Petroli tz (TPDC) nalo likionekana kupigilia kamsumali ka mwisho kina inchi mbili.Kitendawili kilichokuja kuteguliwa na Mzee Magu na Dangote mwenyewe kwa kututhibitishia kuwa; hapakuwa na jambo lolote-kwa maana hiyo zile kauli za akina Muhongo sitaki kuamini kuwa ilikuwa ni Porojo!.
SASA PART2 YAKE IPO HAPA:

Jana asubuhi akihojiwa na BBC mkuu wa kituo cha utafiti wa magonjwa ya binaadamu Tanzania NIMR Dr.Mwela Malecela aliitangazia dunia kwamba; kituo chake kimefanya utafiti katika mikoa ya Morogoro na Geita-kwa kuwapima watu 533 na %15.6 ya watu hao wamekutwa na virusi@dalili za ugonjwa wa ZIKA!.

Ilipofika jioni ya jana hiyohiyo ndani ya saa chache tu Mzee Magu amemtimua kazi Dr.Mwela hii ikiwa na maana ya kwamba ni uongo na uzandiki mkubwa Tanzania hatuna ZIKA kwa mujibu wa Ikulu!.

Ikumbukwe kwamba kituo kile kinao wataalamu wana sayansi wenye uweledi ikijumuishwa na vifaa vyao vya kisayansi vya kupimia binaadamu lakini ukweli wa kile walichodai kukibaini wana sayansi wetu umegeuka kuwa uongo mkubwa mbele ya mkuu wa kaya.

Swali langu bado nalielekeza kwa wizara ya sheria na katiba ikiwamo na wewe rafiki yangu je,bado kuna uhali wa kuendelea kuwaamini mawaziri,wakuu wa taasisi mbalimbali juu ya watakayotueleza bila kuthibitishwa na Ikulu?.

Binafsi hadi sasa nimeanza kushtuka na kukumbwa na woga mkubwa nimeanza kuwa mawazo chanya kwamba yawezekana huko mbeleni tunako elekea (japo sipendi tufike huko) nadhani itafika hatua mtu atakuja kupimwa UKIMWI majibu yakija negativu atadai “SIKUBALI MPAKA IKULU ITHIBITISHE!!

No comments:

Powered by Blogger.