LIVE STREAM ADS

Header Ads

MBAO FC YA JIJINI MWANZA YAMPOTEZA MCHEZAJI WAKE UWANJANI.


Mchezaji wa kikosi cha vijana chini ya miaka 20 katika timu ya soka ya Mbao FC ya Jijini Mwanza, Ismail Mrisho Alfan, amefariki dunia kwenye mechi dhidi ya Mbao FC na Mwadui FC ya Shinyanga katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, ikiwa ni michuano ya vijana kitaifa.

Katika mechi hiyo iliyopigwa jana, mchezaji huyo inaelezwa aligongana na mchezaji mwenzake, beki wa timu ya Mwadu na kwamba aling'ata ulimi baada ya kuanguka chini na kupoteza fahamu kabla ya mauti kumkuta. Kabla ya mauti kumkuta, alikuwa amefunga nao la kuongoza.

BMG tunatoa pole kwa Wana Mbao wote, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wadau wote wa michezo nchini kwa msiba huo. 
#BMGHabari/Mtandaoni

No comments:

Powered by Blogger.