LIVE STREAM ADS

Header Ads

MSUBI BINAGI AWAKUMBUKA WATOTO WANAOLELEWA KITUO CHA SOS CHILDREN'S VILLAGE JIJINI DAR ES SALAAM.

BMGHabari
Disemba Mosi miaka michache iliyopita, alizaliwa, Msubi Binagi, (aliyeweka mkono kifuani) katika wilaya ya Tarime mkoani Mara.


Katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa mwaka huu, leo ametembelea kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha SOS Children's Village kilichopo Mawasiliano Ubungo Jijini Dar es salaam.

Msubi Binagi, kijana mdogo kwenye maono makubwa, amewashukuru ndugu, jamaa na marafiki kwa kuungana naye na hatimaye kufanikisha lengo hilo na amewahimiza wanajamii wengine kuwa na desturi ya kuwasaidia wahitaji katika jamii.

No comments:

Powered by Blogger.