LIVE STREAM ADS

Header Ads

MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM AJA NA TUZO ZA USHAIRI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvatory, BMG Dar
Meya wa jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita, ameandaa mashindano ya tuzo ya ushairi kwa washairi wa jiji hilo yakiwa na lengo la kuhamasisha maendeleo na kuwapa fursa washairi kuhamasisha maendeleo, kuburudisha na kuelimisha.

Mwenyekiti wa tuzo hio, Chatta Michael, amesema zitasaidia kukusanya mashairi na kutengeneza vitabu kwa mataifa na vizazi vijavyo ili kukuza lugha ya kiswahili nchini.

Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa sanaa hiyo imeonekana kurudi chini na haitiliwi mkazo hivyo basi wameamua kushindanisha sanaa hiyo ili iweze kuheshimika kwa mataifa mengine ambayo yanathamini lugha na kuitangaza lugha yetu ya kiswahili kwa mataifa ya ughaibuni.

Pia amefafanua kuwa tuzo hizo zitasaidia washairi kujadili fursa ya maendeleo kwa washairi na kutia mkazo kwa jamii inayowazunguka.

No comments:

Powered by Blogger.