LIVE STREAM ADS

Header Ads

SOKO LA HISA JIJINI DA RE SALAAM LAPAA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Displaying IMG_20161213_102520.jpg
Na James Salvatory, BMG Dar
Mauzo katika soko la hisa la  Dar es Salaam (DSE) yameongezeka mara sita kutoka milioni 198 kwa wiki iliyopita hadi kufikia Tshs.1.22 Bilioni kwa wiki iliyoishia Desemba 9 ya mwaka huu.

Hayo yalibainishwa jana Jijini Dar es Salaam na Afisa  Mwandamizi wa mauzo  wa  (DSE)Marry Kinabo wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Alisema sababu iliyochangia ongezeko hilo la mauzo imetokana na wawekezaji wengi kwenye soko  kuwekeza zaidi kwenye kununua hisa na sio kuwekeza kwenye hati fungani.

Hata hivyo, idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa kwa wiki iliypita yameongezeka  kwa asilimia 44 kutoka wa hisa 262,589 kwa wiki iliyopita hadi kufikia hisa 378,149 kwa wiki hiyo ilishoishia pia Desemab 09,2016.

Kinabo alisema ukubwa mtaji wa soko wa makampuni kwa ujumla umeshuka kwa asilimia 0.5 kwa makampuni ya ndani kwa kuendelea kubaki kiwango kile kile cha trioni nane.

Aliongeza kuwa katika sekta ya viwanda imeshuka kwa point 104.63 na sekta ya huduma za kibenki na fedha imeshuka kwa nukta 3.66 .

Kinabo alizitaja pia kampuni tatu zilizoongoza idadi kwa mauzo ni DSE kwa silimia 47,Benki ya DCB kwa silimia 19 pamoja na kiwanda cha TBL kwa silimia 18

No comments:

Powered by Blogger.