LIVE STREAM ADS

Header Ads

MICHEZO YA TANO YA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA YAPAMBA MOTO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Deudence Kakoko, amewataka wafanyakazi wa mamlaka hiyo kufanya kazi kwa bidii ili kwenda kasi ya  Serikali ya awamu ya Tano.

Akifungua michezo ya tano ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (INTERPORTS GAMES) viwanja vya shule ya Sekondari ya Popatlal Tanga juzi, Kakoko, alisema kila mfanyakazi wa Mamlaka hiyo anapaswa kujua wajibu wake.

Alisema kasi hiyo iende sambamba na uboreshaji wa utoaji huduma bandarini na kuwa kivutio kwa wageni ili kuweza kuitumia kwa kushusha shehena zao bandari za Tanzania.

Michezo hiyo inashirikisha wafanyakazi wachezaji kutoka Tanga ambao ni wenyeji, Dar es Salaam,, Mtwara na Bandari za Ziwa.

Picha na Salim Said

No comments:

Powered by Blogger.