LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM ASEMA NA MACHINGA WA KARIAKOO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

James Salvatory, BMG Dar
Wafanya biashara wadogowadogo maarufu kama (Machinga) wa Soko Kuu la Kariakoo Jijini Da es salaam, wametakiwa kuanzisha mfuko wa kuweka na kukopa (Sacoss) kwa lengo ili kunufaika na fursa mbalimbali ikiwemo mikopo kwa ajili ya biashara zao.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara hao kwenye ziara yake iliyolenga lengo la kusikiliza na kujibu kero zao.

Aidha Makonda kabla ya kuanza kuzungumza na wafanyabiasha  alianza na kuzungumza na viongozi wa soko hilo ambapo alihoji uendeshaji wa soko wake ikiwa ni pamoja na ukusanyaji wa mapato ya soko  hilo  na   kuwaeleza kuwa serikali iko pamoja nao.

Kwa upande wao  machinga hao walipongeza  ujio huo wa Makonda kwani awali walikuwa ikiwemo kutozwa kodi kubwa  ya shilingi 10,000 mpaka 25000 kwa siku changamoto ambayo wanaamini itatatuliwa.

No comments:

Powered by Blogger.