LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWANZA WATAKIWA KUTOENDEKEZA SIASA KWENYE SHUGHULI ZA KINZENGO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Vyama vya siasa mkoani  Mwanza  vimetakiwa, kuacha tabia ya kufanya  shughuli za  zengo  (za kijamii) kisiasa.

Wito huo    ulitolewa jana  na Mjumbe wa Serikali   ya Mtaa  wa Isamilo Kaskazini  A, wilaya ya Nyamagana mkoani humo, Emmanuel Isack.

Isack alisema,  wananchi ambao ni wafuasi wa vyama vya siasa wanatakiwa kuacha kuhusisha mambo ya siasa na shughuli   za  zengo, kwa kufanya hivyo ni  kinyume cha sheria na taratibu. 

Pia alisema, mambo ya siasa  yamekwisha muda wake,muda uliopo ni wakufanya kazi na shughuli za kijamii bila ya kuhusisha itikadi za kisiasa.

Hii ni kutokana na  mjumbe wa serikali za  mtaa huo kupigwa na  wananchi   wanaosadikiwa ni wafuasi wa chama 
cha siasa, waliokuwa wanataka wanazengo wa mtaa huo kutoshiriki maziko,kwenye  msiba uliotokea desemba 14 mwaka huu.

"Naskitika kuona  wananchi   wanaleta mambo ya siasa  kwenye  misiba, kwani nilipata kipigo kutoka  kwa  wafuasi wa  chama kimoja cha siasa, mara baada ya kutokea sintofahamu baina ya nzengo na wafuasi hao," alisema Isack.

Hata hivyo alisema,  kama kuna msiba ni vema kuwaachia wenye msiba na siyo kuleta mambo ambayo  hayahusiani na  sehemu husika.

Kwa  upande wa Mwenyekiti wa Mtaa huo Kombozi Kassim alisema,  kitendo cha kumpiga mjumbe huyo siyo kizuri kwani   kufanya hivyo ni kosa.

Aidha aliwaomba, wananchi   kufanya kazi  kwa bidii kwani maendeleo  hayaji kwa  lelemama na kuacha mambo ya siasa, ambayo muda wake umepita.

"tukiendekeza mambo ya siasa hadi msibani hatuta zikana, kuna watu wengine hawana vyama je hao  watazikwa na nani?" alihoji  kasimu.

No comments:

Powered by Blogger.