LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAARIFA KAMILI KUHUSU UVAMIZI MCHANA KWEUPE JIJINI MWANZA.

KWAMBA TAREHE 30.11.2016 MAJIRA YA SAA 15:00HRS KATIKA MGAHAWA UITWAO DINNERS ULIOPO BARABARA YA KENYATTA KATA NA WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, WATU WAWILI WALIOJULIKANA KWA MAJINA YA;

1.BAGWANI DAKANTE, MIAKA 40, MWENYE ASILI YA ASIA, MHINDI, NA MPISHI WA MGAHAWA WA DINNERS ALIJERUHIWA NA RISASI KWENYE BEGA LA MKONO WA KUSHOTO, NA 2. SULTANI TUGAI, MIAKA 34, MKAZI WA MTAA WA MBUGANI, ALIYEJERUHIWA NA RISASI ILIYOMPARAZA TUMBONI UPANDE WA KUSHOTO  WAKATI WALIPOVAMIWA NA WATU WAWILI  AMBAO NI MAJAMBAZI KATIKA MGAHAWA TAJWA HAPO JUU.

INADAIWA KUWA MAJAMBAZI HAO WALIFIKA KATIKA MGAHAWA HUO WAKIWA KWENYE PIKIPIKI HUKU MMOJA KATI YAO AKIWA AMEVAA KOTI REFU, WALISHUKA NA KUINGIA NDANI YA MGAHAWA  HUO WAKIJIFANYA KUTAKA KUPATIWA HUDUMA YA CHAKULA KAMA WATEJA WENGINE, HUMO NDANI WALIMKUTA  MPISHI BWANA BAGWANI DAKANTE AKIWA NA NDUGU YAKE AITWAYE SURBIR KANTULA WAMEKAA WAKIONGEA KWANI KIPINDI HICHO HUDUMA YA CHAKULA ALIKUWA HAIPO,

NDIPO JAMBAZI MMOJA ALIYEKUWA AMEVAA KOTI ALICHOMOA SILAHA NA KUWATISHIA NA KUWATAKA WATOE PESA, WALIWAPA FUNGUO NA KUWAAMBIA WAKACHUKUE FEDHA KWENYE SANDUKU PINDI MAJAMBAZI WALIPOKUWA WANAHANGAIKIA FUNGUO, NDIPO BAGWANI NA MWENZAKE WALIPOPATA UPENYO NA KUKIMBIA KUPITIA MLANGO WA NYUMA. 

KUTOKANA NA HALI HIYO MAJAMBAZI HAO WALISHITUKA KUWA WANAWEZA WAKAKAMATWA, WALIACHA KUHANGAIKA NA FUNGUO NA KUTAKA KUANZA KUTOKA NDIPO WALIFYATUA RISASI TATU KUELEKEA MLANGO WA MBELE AMBAYO ILIVUNJA KIOO NA KUMPATA BWANA SULTANI TUGAI AMBAYE ALIKUWA NJE,

VILEVILE RISASI NYINGINE ILIMPATA BWANA BAGWANI DAKANTE ALIKUWA TAYARI AMEFIKA MBELE AKIWAELEZA WATU KWAMBA NDANI WAPO WEZI.
MAJAMBAZI HAO WALIFANIKIWA KUTOKA HUMO NDANI NA KUKIMBIA KUTUMIA PIKIPIKI.

AIDHA HAKUNA KITU CHOCHOTE AMBACHO MAJAMBAZI HAO WAMEPORA KATIKA ENEO LA TUKIO, UPELELEZI MKALI UNAFANYIKA SEHEMU ZOTE ILI KUHAKIKISHA MAJAMBAZI HAO WANATIWA NGUVUNI, TAYARI WATU WANNE WAMEKAMATWA KWA MAHOJIANO, MAJERUHI MMOJA AMELAZWA HOSPITALI YA CF NA MWINGINE AMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO WAKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU, HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA WATULIE, HUKU WAKIENDELEE KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LAO LA POLISI ILI WATU HAO AMBAO WAMEIBUKA WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.

ALIONGEZA KUWA ENDAPO WANANCHI WATAKUWA KITU KIMOJA NA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA ZA MAJAMBAZI HAO BASI TUTAWEZA KUKOMESHA UHALIFU KATIKA MKOA WA MWANZA KWA MUDA MFUPI.

IMETOLEWA NA: DCP: AHMED MSANGI KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

No comments:

Powered by Blogger.