TPDC WATOLEA UFAFANUZI MALALAMIKO YA KIWANDA CHA DANGOTE MTWARA.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvatory, BMG Dar
Shirika la Maendeleo ya Petrol nchini (TPDC) limekanusha taarifa zinazoenezwa na kampuni ya Dangote pamoja na washirika wake kupitia mitandao ya kijamii pamoja na vyombo vya habari zilizokuwa zikidai kuwa TPDC imeshindwa kukiuzia gesi asilia kwa bei rahisi kiwanda cha saruji cha dangote kilichopo mkoani mtwara na hivyo kuwa moja ya sababu ya kusimamisha uzalishaji wa saruji katika kiwanda hicho.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es salaam kaimu mkurugezi mtendaji wa TPDC mhandisi Kapuulya Msombi amesema kuwa si sahihi kusema TPDC imemkwamisha Dangote katika uzalishaji wa Saruji Mkoani Mtwara na kusema taarifa hizo hazina mantiki yoyote na zinapaswa kupuuzwa kwani TPDC imefanya jitihada za kuhahikisha kwamba kampuni ya Dangote inaendelea na uzalishaji wa saruji kama ilivyokusudiwa.
Aidha mhandisi Msombi amesema kuwa wamefanya jitihada mbalimbali kuhakikisha kampuni ya Dangote inapata nishati hiyo kwa ajili ya kuzalisha saruji , ikiwemo kufanyika kwa vikao mbalimbali pamoja na makubaliano yaliyofanyika kwa Dangote kuridhia nia yao ya kutumia ges asilia kuzalisha umeme kwa ajili ya kiwanda cha saruji cha dangote kilichopo mkoani Mtwara.
“TPDC hufuata kanuni na utaratibu wa kupanga bei ya ges asilia ambapo hupanga kulingana na aina ya wateja ambapo Wateja wamegawanyika kufuatia makundi tofauti kama vile wateja wa viwandani, majumbani ,magari pamoja na wateja wa kuzalisha umeme hata hivyo bei elekezi ambayo inakua inapendekezwa na TPDC lazima iridhiwe na ipitishwe na EWURA ndiyo ianze kutumika alisema,”alisema Msombi.
Aidha msombi amesema kuwa TPDC hufuata kanuni na utaratibu kwa kupanga bei ya gesi asilia ambapo hupanga kulingana na aina ya mteja.
“Kiwanda cha Dangote kimeomba kupewa gesi asilia kwa bei ambayo hapa kwetu Tanzania ni kidogo kwani kiasi hicho cha bei ndicho kinacholipwa kununulia gesi ghafi kutoka kisimani hivyo basi ,TPDC haiwezi kuuza gesi asilia kwa bei ya kisima kwa sababu kuna gharama zinazoongezeka katikakuisafisha na kusafirisha gesi hiyo
“TPDC imefanya majadiliano ya mkataba ya awali na Kiwanda cha Saruji cha Dangote kwa ajili ya kuwauzia gesi asilia itakayotumika kuzalishia umeme utakaotumiwa na kiwanda hicho. Inategemewa hadi kufikia mwezi Januari 2017 miundombinu ya gesi asilia itakua imeshaunganishwa na mitambo ya kufua umeme utakaotumiwa na Kiwanda hicho.

No comments: