LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANAWAKE MKOANI MWANZA WAZINDUA UNGA WA VIAZI LISHE.


#BMGHabari
SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA, WANAWAKE WAJASIRIAMALI MKOANI MWANZA WAZINDUA UNGA WA VIAZI LISHE ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI.
Mbunge wa Viti Maalumu Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Kiteto Koshuma, amefungua Kongamano la Wanawake Wajasiriamali mkoani Mwanza, linalofanyika Jijini Mwanza hii leo ambapo pamoja na mambo mengine, unafanyika uzinduzi wa Unga wa Viazi Lishe.

Koshuma amesema akina mama wakijishughulisha kiuchumi, wataweza kuepukana na manyanyaso katika Jamii.
Viazi lishe ni zao linalostawi vyema na hutengeneza bidhaa mbalimbali kama chapati, mandazi, biskuti ambapo pia viazi hivyo hutumika kama chakula chenye vitamini A kinachosaidia kuepukana na upofu.

Hongera Shirika la Tanzania Entrepreneur Development & Advocacy Organization TEDA pamoja na Sauti ya Wanawake kutoka Ukerewe miongoni mwa mashirika mengine ikiwemo Agri_Business Media Initiative in Tanzania kwa kusaidia uzalishaji wa zao la Viazi lishe mkoani Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.