LIVE STREAM ADS

Header Ads

HECHE ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA CHADEMA KANDA YA SERENGETI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Ijumaa Januari 20,2017 kumefanyika mkutano mkuu maalumu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga,Mara na Simiyu umefanyika katika ukumbi wa mikutano Karena Hotel Mjini Shinyanga.

Viongozi mbalimbali wa kitaifa wa CHADEMA wamehudhuria mkutano huo ambao umeenda sambamba na kufanya uchaguzi wa viongozi wa kanda ya Serengeti ambapo John Heche amechaguliwa kuwa mwenyekiti,Gimbi Masaba kuwa makamu mwenyekiti n Catherine Ruge kuwa mweka hazina.

Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Freeman Mbowe ametumia mkutano hiyo kutoa ujumbe kwa taifa kupitia vyombo vya habari.
Mbowe amesema nchi ya Tanzania inapitia changamoto nyingi kwa kipindi hiki lakini kubwa zaidi kuliko yote ni hofu inayotamalaki ndani ya taifa kwamba watu wameanza kujiona kuwa hawako salama sana ndani ya nchi yao.

Amesema kuna watu ambao wana hofu ya njaa,hofu ya kuporomoka kwa uchumi,hofu za kiusalama,lakini CHADEMA ina hofu kubwa kuhusu usalama wa viongozi wake,hofu kubwa kuhusu kutokutendewa haki viongozi wa cha hicho kuanzia viongozi wa kitaifa,kwenda kwa wabunge,madiwani,wenyeviti wa vijiji,wenyeviti wa mitaa hata na vitongoji pamoja na wanachama wao.

“Badala ya kujengwa hofu ni lazima sasa tusimamie imara kuijenga CHADEMA yenye nguvu kujenga upinzani wenye nguvu,kusimama kwa haki bila kuogopa”,amesema Mbowe.
“Ni juzi tu rais amemteua wabunge wengine katika orodha ya wabunge 10 anaoweza kuwateua,katiba ya nchi inasema anapaswa ateue 10,lakini kati yao wasipungue wanawake watano,lakini hadi jana rais ameshateua wabunge nane kati yao sita ni wanaume kwa maana hiyo tayari ameshavunja katiba”,anasema Mbowe.
SIKILIZA HAPA HOTUBA YA DAKIKA 13 ILIYOTOLEWA NA MWENYEKITI WA CHADEMA TAIFA FREEMAN MBOWE AKIWA SHINYANGA IJUMAA JANUARI 20,2017

Kushoto ni mwenyekiti wa Chadema taifa Freeman  Mbowe,katikati ni katibu mkuu wa Chadema Vicent Mashinji na naibu katibu mkuu Chadema bara John Mnyika wakiteta jambo wakati wa mkutano maalum wa Chadema kanda ya Serengeti uliofanyika katika ukumbi wa Karena Hotel mjini Shinyanga
Wa kwanza kushoto ni Makamu mwenyekiti Chadema taifa Zanzibar,Said Issa Mohammed.Wa kwanza kulia ni naibu katibu mkuu Chadema taifa Zanzibar Salum Mwalim
Viongozi mbalimbali wa Chadema taifa wakiwa ukumbini
Viongozi wa Chadema wakiwa ukumbini
Viongozi wa Chadema wakiwa meza kuu
Wajumbe wa mkutano wakiwa ukumbini
Katibu mkuu wa Chadema taifa Vicent Mashinji akizungumza ukumbini ambapo alisema vitendo mbalimbali wanavyofanyiwa viongozi wa chama hicho ni ishara kubwa kuwa ushindi wa chama hicho umekaribia
Wajumbe wa mkutano huo wakiwa ukumbini
Katibu mkuu wa Chadema Vicent Mashinji akizungumza
Mwenyekiti wa Chadema taifa Freeman Mbowe akitoa ujumbe kwa taifa kuhusu hali ya nchi ya Tanzania hivi sasa
Mwenyekiti wa Chadema taifa Freeman Mbowe akizungumza ukumbini.Waliokaa kushoto ni wagombea katika uchaguzi wa viongozi Chadema kanda ya Serengeti 
Katibu mkuu wa Chadema Vicent Mashinji akisoma katiba ya nchi.
Wajumbe wa mkutano wakimsikiliza mwenyekiti wao
Mwenyekiti wa Chadema taifa Freeman Mbowe akisisitiza jambo
Wajumbe wa mkutano wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
UCHAGUZI KANDA YA ZIWA VICTORIA

No comments:

Powered by Blogger.