LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAADHIMISHO YA MIAKA 40 YA KUZALIWA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com


Chama cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga Mjini katika mkoa wa Shinyanga kimefanya Kongamano ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya Maadhimisho ya miaka 40 tangu kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM tarehe 05.02.1977.


Kongamano hilo lilifanyika jana katika Ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Shinyanga mjini na mkoa wa Shinyanga,makada wa CCM na vyama vya upinzani na watu mbalimbali wenye mapenzi mema wakiwemo wanafunzi wa Shule ya sekondari Buluba na Kom sekondari.

Mada mbalimbali zilitolewa wakati wa kongamano hilo ikiwemo historia ya CCM na mafanikio ya chama hicho tangu kuanzishwa kwake mwaka 1977.

Katika kuadhimisha wiki ya maadhimisho ya miaka 40 ya CCM,Chama cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga kitashiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika ngazi ya matawi ikiwemo,kupanda miti,kusalimia wagonjwa,watoto yatima,walemavu,kutembelea shule,michezo na kufanya mikutano ya ndani badala ya mikutano ya hadhara.

Vyama asili vilivyozaa CCM ni Tanganyika African National Union (TANU) cha Tanganyika  na Afro Shiraz Party (ASP) cha Zanzibar vyote vikiwa ni vyama vya ukombozi.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 40 ya CCM ni "CCM Mpya,Tanzania Mpya".
Viongozi mbalimbali wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini na mkoa wa Shinyanga wakiwa meza kuu.Wa kwanza kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangura,akifuatiwa na naibu meya wa manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya,Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Alhaj Saad Kusilawe,mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu Tajiri Maulid na meya mstaafu wa manispaa ya Shinyanga ambaye sasa ni diwani wa Kata ya Kambarage Hassan Mwendapole
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangura akizungumza wakati wa kongamano hilo ambapo alisema katika kusherehekea miaka 40 ya CCM watashiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo sambamba na kufanya mikutano ya ndani badala ya mikutano ya hadhara
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu Tajiri Maulid akisitiza jambo ukumbini
Wanachama wa CCM wakiwa ukumbini
Wanafunzi wa shule ya sekondari KOM wakiwa na mwalimu wao ukumbini wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Viongozi mbalimbali wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa ukumbini
Wafuasi wa CCM wakiwa ukumbini
Tunafuatilia kinachoendelea ukumbini
Mwalimu Patrick Kija alitoa mada kuhusu historia ya Chama Cha Mapinduzi na kuelezea harakati za ukombozi kutoka enzi za ukoloni
Aliyekuwa katibu tawala wa CCM mkoa wa Shinyanga Abdul Dachi akichangia mada kuhusu historia ya Chama Cha Mapinduzi
Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Alhaj Saad Kusilawe akitoa mada kuhusu mafanikio ya CCM tangu kianzishwe mpaka sasa.Alisema hata Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umeimarika zaidi
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu Tajiri Maulid,mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa na diwani wa kata ya Kambarage Hassan Mwendapole wakifuatilia kwa umakini kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Tunafuatilia kinachoendelea
Meya mstaafu wa manispaa ya Shinyanga ambaye sasa ni diwani wa Kata ya Kambarage Hassan Mwendapole akionesha ilani ya uchaguzi ya 2015 ya CCM wakati akitoa mada kuhusu mafanikio ya CCM katika awamu ya tano inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli.
Mwanachama wa CCM Joseph Maige akichangia hoja ukumbini
Mkuu wa wilaya mstaafu Zipporah Pangani akichangia hoja wakati wa kongamano hilo ambapo aliomba Chama Cha Mapinduzi kijikite katika kutoa elimu juu ya ilani ya uchaguzi ya chama hicho sambamba na kuimarisha chama katika ngazi ya matawi
Mwanafunzi Mariam Mrisho anayesoma kidato cha tano katika shule ya sekondari Buluba iliyopo mjini Shinyanga akichangia hoja katika kongamano hilo
Mwenyekiti wa CCM mko wa Shinyanga Erasto Kwilasa akifunga kongamano hilo ambapo aliwasititiza wanachama wa CCM kutoendekeza makundi ndani ya chama
Na Kadama Malunde-Malunde1 blog

No comments:

Powered by Blogger.