SOKO JIPYA LA TAMBUKA RELI KUONGEZA NEEMA KWA WAKAZI WA BUTIMBA JIJINI MWANZA.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Ujenzi wa Soko jipya la Tambuka Reli lililopo katika Kata ya Butimba Jijini Mwanza, unatarajia kukamilika ambapo ajira zaidi ya 200 zitapatikana kwa wakazi wa ndani na nje ya kata hiyo.
Diwani wa Kata hiyo, John Pambalu, jana aliiambia Lake Fm Mwanza kwamba, soko hilo linatarajiwa kugharimu takribani shilingi milioni 500 hadi kukamilika kwake ikiwa ni nguvu za wananchi pamoja na halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Alisema wananchi zaidi ya 200 wameisha inua maboma na kuyaezeka katika soko hilo huku kukiwa na nafasi za vyumba 42 ambazo wamiliki wake walishindwa kuziendeleza na tayari tenda imetangazwa ambapo amewahimiza wakazi wa kata ya Butimba kuchangamkia fursa hiyo.
Pambalu alibainisha kwamba kuna soko hilo litawanufaisha wananchi wapatao 800 ambao ni pamoja na wafanyabiashara na wasaidizi wao na hata wauzaji wa bidhaa na mazo mbalimbali.
Bonyeza Hapa Au play hapo chini kusikiliza sauti.
Diwani wa Kata ya Butimba Jijini Mwanza, John Pambalu (Chadema), akizungumza kwenye moja ya mikutano ya chama hivi karibuni wilayani Nyamagana.
LakeFmHabariUjenzi wa Soko jipya la Tambuka Reli lililopo katika Kata ya Butimba Jijini Mwanza, unatarajia kukamilika ambapo ajira zaidi ya 200 zitapatikana kwa wakazi wa ndani na nje ya kata hiyo.

No comments: