LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

KATIKA TUKIO LA KWANZA,
KWAMBA TAREHE 23.01.2017 MAJIRA YA SAA 20:00HRS USIKU KATIKA KIJIJI CHA IGOMBE “A” KATA YA BUGOGWA WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA KIJANA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA PETRO MAGAYANE MIAKA 22, MKEREWE NA MKAZI WA IGOMBE, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUMBAKA NA KUMJERUHI KATIKA SEHEMU ZAKE ZA SIRI MTOTO JINA TUNALIHIFADHI MWENYE UMRI WA MIAKA 5, MKAZI WA IGOMBE, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.

INADAIWA KUWA MAJIRA TAJWA HAPO JUU MTUHUMIWA AKIWA AMELEWA  ALIFIKA MAENEO YA NYUMBANI ANAPOISHI MTOTO HUYO KISHA AKAMTUMA DUKANI MAENEO YA MWALONI IGOMBE, AIDHA BAADA YA MUDA MCHACHE KUPITA MTUHUMIWA ALIMFUATA MTOTO HUKO DUKANI MWALONI IGOMBE KISHA KUMFANYIA UKATILI WA KUMBAKA NA KUSABABISHA MAJERAHA NA MAUMIVU MAKALI KATIKA SEHEMU ZA SIRI ZA MTOTO HUYO.

WANANCHI WALITOA TAARIFA POLISI KUHUSIANA NA TUKIO HILO, ASKARI WALIFIKA ENEO LA TUKIO NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA. MTUHUMIWA YUPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI. AIDHA UCHUNGUZI WA AWALI UNAONESHA CHANZO CHA TUKIO HILI NI ULEVI. MTOTO AMEPATIWA MATIBABU HOSPITALI NA HALI YAKE INAENDELEA VIZURI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI/ WALEZI AKIWATAKA KUWA MAKINI WAKATI WOTE NA WATOTO ILI KUWAEPUSHA NA WATU WENYE NIA OVU DHIDI YAO, AIDHA ANAWATAKA BAADHI YA WATU WENYE TABIA YA ULEVI WA KUPINDUKIA AMABO UNAPELEKEA KUFANYA VITENDO VYA UHALIFU WA AINA KAMA HII KUACHA MARA MOJA KWANI IKIBAINIKA HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAO.

KATIKA TUKIO LA PILI,
MNAMO TAREHE 23.01.2017 MAJIRA YA SAA 09:00HRS ASUBUHI KATIKA KIJIJI CHA NYAHONGE KATA YA FUKALO WILAYA YA KWIMBA MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA JOSEPH MAFURAYA MIAKA 45, MSUKUMA NA MKAZI WA KIJIJI CHA MALYUNGU ALIGUNDULIKA KUWA AMEFARIKI DUNIA NYUMBANI KWA SHAGEMBE LYANDOLA MIAKA 49, MKAZI WA NYAHONGE AMBAPO ALIFIKA KUNYWA POMBE AINA YA GONGO  MAHALI HAPO.

INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIFIKA  NYUMBANI KWA SHAGEMBE LYANDOLA AKITOKEA KIJIJI CHA MALYUNGU AKIWA AMEKUNYWA POMBE YA GONGO NA ALIPOFIKA  MAHALI HAPO AMBAPO NAPO WALIKUWA WAKIUZA POMBE HIYO KWA SIRI,  ALIOMBA AHUDUMIWE POMBE HIYO. AIDHA INASEMEKANA KUWA WAKATI MAREHEMU AKIWA NA WENZAKE WAKIENDELEA KUNYWA POMBE MAHALI HAPO GHAFLA ALIANGUKA CHINI NA KUPOTEZA FAHAMU KISHA KUFARIKI DUNIA MUDA MCHACHE BAADAE.

WATU WALITOA TAARIFA POLISI KUHUSIANA NA KIFO HICHO, ASKARI WALIFIKA MAPEMA ENEO LA TUKIO NA KUMKUTA MAREHEMU AKIWA TAYARI AMEFARIKI DUNIA. AIDHA UCHUNGUZI WA AWALI UNAONESHA KUWA CHANZO CHA KIFO CHAKE NI KUWA ALIKUNYWA POMBE AINA YA GONGO BILA KULA CHAKULA KWA MUDA MREFU, UPELELEZI WA KIFO HICHO BADO UNAENDELEA, MWILI WA MAREHEMU TAYARI UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI NA KUKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA, AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUNYWA AU KUTENGENEZA POMBE HARAMU YA GONGO KWANI KOSA LA JINAI, LAKINI PIA ANAWAOMBA WANANCHI KUTOA TAARIFA POLISI ZA WATU WANAOTENGENEZA NA KUUZA POMBE HIYO ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUWAFIKISHA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.

KATIKA TUKIO LA TATU,
MANAMO TAREEHE 23.01.2017 MAJIRA YA SAA 14:20HRS MCHANA KATIKA KIJIJI CHA IGOMBE WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKIWA DORIA NA MISAKO WALIFANIKIWA KUWAKAMATA WATU WAWILI WALIOJULIKANA KWA MAJINA YA 1.BAHATI MWIZALWA, MIAKA 44, MKEREWE, MFANYABIASHARA, AMEKAMATWA AKIWA NA POMBE YA MOSHI (GONGO) KIASI CHA LITA 200 NA MTAMBO MMOJA WA KUTENGENEZEA POMBE HIYO PAMOJA NA SUKARI KILO 50, MALI IDHANIWAYO KUWA YA WIZI NA 2. NEEMA MANJALE MIAKA 20, MKURIA, MKAZI WA KIJIJI CHA IGOMBE, YEYE AMEKAMATWA AKIWA NA POMBE AINA YA GONGO KIASI CHA LITA 20, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.

AWALI ASKARI WAKIWA KATIKA DORIA NA MISAKO WALIPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA JUU YA UWEPO WA WATU AMBAO WANAJIHUSISHA NA UTENGENEZAJI PAMOJA NA UUZAJI WA POMBE HARAMU YA GONGO KIJIJINI HAPO, ASKARI WALIFIKA HADI NYUMBANI KWA WASHUKIWA NA KUFANYA UPEKUZI NA KUFANIKIWA KUWAKAMATA WATUHUMIWA TAJWA HAPO JUU WAKIWA NA POMBE HIYO HARAMU YA GONGO PAMOJA NA KILO 50 ZA SUKURI MALI IDHANIWAYO KUWA YA WIZI KWANI HAKUWA NA NYARAKA YEYOTE INAYOTHIBITISHA UHALALI WA KUMILIKI SUKARI HIYO.

WATUHUMIWA WAPO KATIKA MAHOJIANO NA POLISI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI, JESHI LA POLISI BADO LINAENDELEA NA MISAKO PAMOJA NA UKAMATAJI WA WATU WOTE AMBAO WANAENDELEA NA UTENGENEZAJI PAMOJA  NA UUZAJI WA POMBE HARAMU YA GONGO.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA WATOE USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KUHUSIANA NA WATU AMBAO WANAJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA POMBE YA GONGO ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.

IMETOLEWA NA,
DCP: AHMED MSANGI

KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

No comments:

Powered by Blogger.