LIVE STREAM ADS

Header Ads

WADAU WA MICHEZO MKOANI MWANZA WACHANGIA UKARABATI WA UWANJA WA CCM KIRUMBA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza 
Baadhi ya wadau michezo mkoani Mwanza wameanza kujitokeza na kuchangia mifuko 25 ya saruji kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya kupitisha maji taka katika eneo la uwanja wa CCM Kirumba. 

Meneja wa uwanja huo, Steven Shija, ameiambia BMG kwamba waliochangia ni pamoja na Moshi Balukuli (Mjasiriamali) aliyechangia saruji mifuko 10, Jamal Abdul Babu (MNEC Nyamagana) aliyetoa saruji mifuko mitano na Mbunge wa jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula aliyechangia saruji mifuko 10.

Aidha Shija amesema bado mifuko 75 ya saruji inayohitajika ili kukamilisha ujenzi wa miundombinu hiyo ambapo amewasihi wadau mbalimbali wa michezo kuendelea kujitokeza kusaidia ukarabati huo kwa ajili ya maendeleo ya michezo mkoani Mwanza. Tazama picha hapa

No comments:

Powered by Blogger.