TAASISI YA AMI-TZ YA JIJINI MWANZA YAWAHIMIZA WAJASIRIAMALI KUFUNGASHA MAZAO YAO.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Wajasiriamali wanaojihusha na shughuli za kilimo cha matunda na mbogamboga nchini, wamehimizwa kufungasha mazao yao na kuwafikishia wateja wao badala ya kusubiri wayafuate shambani.
Mjasiriamali na Mkurugenzi wa taasisi ya kilimo ya Agro-Busness Media Initiative ya Jijini Mwanza, Deborah Mallaba, ametoa ushauri huo wakati akizungumza na Lake Fm juu ya manufaa ya kilimo cha mbogamboga na matunda.
Amebainisha kuwa kilimo hicho kina faida kubwa ikiwa mkulima atazingatia kanuni bora za kilimo na kwamba huwa anafungasha mazao yake na kuwafikishia wateja majumbani na maofisini badala ya kusubiri wayafuate shambani na hivyo kuondokana na hasara ya mazao kuharibika yakiwa shambani jambo ambalo pia humuongezea zaidi kipato.
Mallaba amewahimiza akina mama na vijana kujikita kwenye kilimo cha biashara kwani kina manufaa makubwa badala ya kutegemea ajira za maofisini pekee huku akiwahimiza kutembelea shamba darasa la taasisi yake lililopo Igombe ziwani katika Manispaa ya Ilemela ili kujifunza zaidi kuhusu kilimo bora.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Agri-Busness Media Initiative In Tanzania (AMI-TZ) ya Jijini Mwanza, Deborah Mallaba, akikagua shamba la hekari mbili la taasisi hiyo ambalo lina mkusanyiko wa matunda na mbogamboga za aina mbalimbali, lililopo Igombe Ziwani, Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.
Kwa msaada na ushauri, piga simu nambari 0754 99 66 13
No comments: