LIVE STREAM ADS

Header Ads

TIMU YA SOKA YA MBAO FC YA JIJINI MWANZA YAKUNJUA MAKALI YAKE.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Timu ya Mbao Fc ya Jijini Mwanza, imeigaragaza timu ya Ruvu Shooting, kwa kuifunga goli 2-0, katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania (VLP).

Katika mchezo huo uliochezwa jana katika uwanja wa CCM Kirumba, Mbao Fc ambao walikuwa katika uwanja wa nyumbani,walionekana kuwazidi mbinu wapinzani wao Ruvu Shooting.

Mbao Fc walifunga magoli kipindi cha kwanza kupitia washambuliaji wake Habib Haji (17) dakika ya 17 na Dickson Ambundo (7) dakika ya 21.

Kupitia ushindi huo Mbao Fc imekuwa na jumla ya pointi 23 wakiwa nyuma ya Ruvu Shooting kwa pointi moja.

Kwa upande wake Kocha wa Mbao Fc Etienne Ndairahije alisema,anamshukuru Mungu kwa kujipatia pointi 3 nyumbani.

Naye  Kocha wa Ruvu Shooting Malale Hamsini alisema, hawajazidiwa  na wapinzani wao,ila walishindwa kutumia nafasi walizokuwa wanapata.

Hata hivyo alisema, watarekebisha makosa na wanajipanga na mechi mbili kati ya Toto Afrika na Mwadui Fc.

No comments:

Powered by Blogger.