LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO JIJINI MWANZA WAUGOMEA TIMU YA TOTO AFRIKA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Katika hali ya kushangaza, waandishi wa habari za michezo kutoka vyombo mbalimbali mkoani Mwanza, wamejikuta wakiambulia matusi na maneno ya kashifa kutoka kwa baadhi ya viongozi na wanachama wa timu ya Toto Afrika.

Sintofahamu hiyo ilitokea jana wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bar kati ya Mbao Fc na Ruvu Shooting katika Uwanja wa CCM Kirumba.

"Nyie waandishi uchwara, mbona hamuandiki habari zinazoihusu Toto?" Mmoja wa mashabiki hao alisikika.

Mwandishi wa Clouds FM Fanuel Fabian alisema lugha walizotumia viongozi hao siyo nzuri na zimewadharirisha huku Sheila Katikula, mwandishi wa gazeti Mtanzania akiwataka wadau wa michezo na jamii kwa ujumla kuacha kuwadharau waandishi na kuheshimu kazi hiyo.

Hata hivyo baada ya kumalizika mchezo huo, waandishi hao waliuita uongozi wa timu hiyo ili kufikisha malalamiko yao lakini waligoma na hivyo waandishi hao wamedhamiria kutoandika habari zinazoihusu timu ya Toto Afrika.

No comments:

Powered by Blogger.