LIVE STREAM ADS

Header Ads

HATUA ZILIZOFIKIWA KWENYE ZOEZI LA UOKOAJI KATIKA MGODI ULIOANGUKA MKOANI GEITA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com


Zoezi la uokoaji likiendelea huku bomba za kupitisha hewa ya Oxgen zikiwa zimepitishwa chini kwa chini ili kupeleka hewa kwa wahanga walioangukiwa na mgodi wa RZ mkoani Geita.
MadukaOnline
Ni siku ya tatu leo tangu wachimbaji 15 kuangukiwa na mgodi wa RZ uliopo Kijiji cha Nyarugusu mkoani Geita na kuibua simanzi na masikitiko makubwa kwa ndugu jamaa na marafiki licha ya kwamba jitihada na zoezi la kuwaokoa bado linaendelea.

Zoezi la uokoaji linalosimamiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoani humo, Ofisi ya Madini Kanda ya ziwa magharibi ikiyashirikisha makampuni ya Migodi ikiwemo GGM  na Busolwa Mine, imeelezwa hatua iliyofikiwa hadi jana kwamba ni kuchimba takribani mita 20 kati ya 30 ili kuwafikia wachimbaji hao.

Kufuatia hatua hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga aliwataka  ndugu na jamaa wa watu 14 waliofukiwa na kifusi ndani ya Mgodi wa RZ   kuwa na subira wakati waokoaji wakiendelea na Zoezi hilo.

 Aidha Mkuu huyo wa Mkoa ametoa  kalipio kali kwa wawekezaji ambao hawajali ustawi wa wafanyakazi wake kwa uzembe ambao unaweza kuepukika na kwamba alisikitishwa sana namna mgodi wa RZ ambavyo ulikuwa haujali masuala ya miundombinu yake.

Zoezi la uokoaji limeendelea huku matumaini ya wengi yakizidi kupotea kutokana na ugumu wa kazi dalili hata kidogo hazionekani lakini kamishina wa madini kanda ya ziwa magharibi Bw. Yahaya Samamba amesema zoezi hilo litakamilika na watu watakuwa salama kutokana na hewa wanayoipata kupitia mpira unaoingiza kwa kutumia mashine.

Kamishina msaidizi wa  madini kanda ya Ziwa  Yahaya Samamba ameendelea kuelezea kuwa  pamoja na kuunda kamati ya uokoji wamekutana na changamoto kubwa kwa sababu ya duara walikozama watu hao kuwa chini ya kilomita 35.huku akisema wanaendelea kuomba mashine nyingine kutoka kwa makampuni mengine kama zoezi litaonekana kuwa na ugumu.

Diwani wa kata ya Nyarugusu yalipo maafa hayo, Swalehe Juma  alisema janga hilo limemnyima usingizi na kwamba siku ya jana alilazimika kukesha na waokoaji.

 Hata hivyo baadhi ya wananchi waliohudhuria kushuhudia tukio hili la aina yake katika wilaya ya Geita ikiwa ni mwanzoni mwa mwaka wa 2017, walisema lawama kubwa wanazielekeza kwa mamlaka za madini kwa kushindwa kujisimamia katika kuhakikisha uchimbaji ulio imara kwenye migodi unaboreshwa.

Katika shughuli za uokoaji wananchi hawakuacha kuipongeza kampuni ya uchimbaji wa madini ya Busolwa Mine inayomilikiwa na mwekezaji mzawa Baraka kwa kujitolea mashine zake za greda kuhakikisha wanafanikisha adhima ya kuwaokoa watanzania 13 pamoja na raia wa china Bw. Meng Juping, ambaye anadaiwa hakuwa na redio koll kama ilivyokuwa kawaida yake wakati anakwenda kutekeleza majukumu yake ya uzalishaji wa madini ya dhahabu.

No comments:

Powered by Blogger.